Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:23

UNHCR yaitahadharisha Washington isikiuke sheria za kimataifa


Mama mhamiaji wa Honduras na mtoto wake wakivuka daraja baada ya kuvuka mpaka ulioko kati ya Guatemala and Mexico, katika mji wa Ciudad Hidalgo, Mexico, Octoba 20, 2018.
Mama mhamiaji wa Honduras na mtoto wake wakivuka daraja baada ya kuvuka mpaka ulioko kati ya Guatemala and Mexico, katika mji wa Ciudad Hidalgo, Mexico, Octoba 20, 2018.

Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) linalo washughulikia wakimbizi (UNHCR), imeitahadharisha Washington iko katika ukingo wa kukiuka sheria za kimataifa kwa kuwazuia watu wanaohitaji hifadhi kuingia Marekani.

Wakati karibu watu elfu tatu wamezuiliwa kwenye mpaka kati ya Mexico na Guatemala, Shirika hilo linaendelea kusisitiza kuwa watu wanaokimbia unyanyasaji na uvunjifu wa amani wanahaki ya kulindwa kimataifa

Kauli hii inafuatia tishio la Rais Donald Trump kwa mexico na Hondurus kwamba Washington itasitisha misaada yake kwa nchi hizo na hapo jana kwenye ujumbe wake wa tweeter kiongozi huyo amesema juhudi kamili zinachukuliwa kuzuia maelfu ya wahondurus kuingiaMarekani.

Amesema msafara huo wa watu ni aibu kwa chama cha Democrats. Badilisheni sheria za uhamiaji.”

Wahamiaji wakaidi vitisho vya Marekani

Hayo yote yakitokea wahamiaji wamekaidi vitisho vya Trump na matifa manne waliopitia hadi kufika kwenye daraja la kuingia Mexico kutoka Guatemala.

Baada ya kuzuiliwa kwa siku nne kuna wale ambao wamewalipa wamiliki wa mitumbwi dola moja unusu kuwavusha mto kuingia Mexico, nakuna wale wanawake na watoto waloruhusiwa kuvuka mipaka na maafisa wa Mexico pia wameanza kuwaorodhesha baadhi na kuwapatia hati za kusikiliza kesi zao za ukimbizi.

Mhamiaji mwenye ulemavu kwenye kiti cha Sergio Cazeres anasema hakuna njia ya kurudi nyumbani Hondurus.

Sergio Cazeres Mhamiaji kutoka Hondurus

Serikali ya Hoduras hapana kitu, haimsaidi mtu yeyote. Hata sisi walemavu ndio kabisa hawatusaidi. Waangaliye watu hawa wote hawana kazi, wanakimbia nchi kutokana na shida tupu.

Hata hivyo kuna baadhi walokata tamaa na kuanza kurudi nyumbani kwa mabasi ya kiraia na kijeshi yaliyotolewa na Guatemala na Hondurus.

Mkutano wa marais

Marais wa Hondurus na Guatemala walikutana mwishoni mwa wiki mjini Guatemala City kuzungumzia tatizo hilo na Rais wa Guetamala Jimmy Morales akiwa pamoja na mwenzake Juan Orlando wa Hondurus amesema watu elfu mbili wamesharudi nyumbani.

Rais Morales amesema Kati ya watu elfu 5 hadi elfu 5 mia nne waliingia Guatemala. Na vile vile tuna idadi ya awali ya watu elfu 2 au karibu ya idadi hiyo ambao wamehesabiwa kurudi Hondurus kwa salama.

Wengine walobaki wameweka kambini katika mji karibu na daraja la kuingia Mexico wakipumzika na kupatiwa matibabu hasa majeraha ya miguu kutokana na kutembea karibu kilomita 700 kutoka mji wa San Pedro Sula kaskazini ya Hondurus.

Shirika la Msalaba Mwekundu

Kulingana na wafanyakazi wa msalaba mwekundu wengi wana matatiuzo ya tumbo kutokana na kutokula kwa siku kadhaa na upungufu wa maji mwilini.

Safari iliyobaki kufika mpaka wa Mexico na Marekani ni umbali wa kilomita elfu 3 na kuna waliokubaliwa kuingia na kuchukuliwa na mabasi lakini mfanyakazi wa shirika la huduma za wahamiaji Flor Cedrel anasema watu wanamahitaji makubwa.

Shirika la UNHCR

Flor Cedrel, Mfanyakazi wa Shirika la huduma za wahamiaji (UNHCR), anaeleza bila shaka watu wanahangaika. Hawaruhusu kuvuka wamekwama kwenye daraja. Hatujui ni watu wangapi wameweza kuvuka na wako wapi. Hatujui wameahidiwa wanapelekwa wapi baada ya kupandishwa kwenye mabasi.

Wale wasiovunjika moyo wanatumia kila njia wawezayo kuvuka ikiwa kutembea kwenye mto au kuchupa kutoka daraja ilimuradi wanasema wataendelea na safari yao. Huku mashirika ya huduma za kiraia zinawasaidia kwa chakula na misaada ya dharura.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Abdushakur Aboud, Washington, DC

XS
SM
MD
LG