Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 11:53

Mkataba wa Nyuklia : Trump ailaumu Russia


Rais wa Marekani Ronald Reagan (kulia) na Rais wa Soviet Mikhail Gorbachev wakisaini mkataba wa INF) White House, Disemba 8 1987.
Rais wa Marekani Ronald Reagan (kulia) na Rais wa Soviet Mikhail Gorbachev wakisaini mkataba wa INF) White House, Disemba 8 1987.

Rais wa Marekani Donald Trump amesema ataiondosha Marekani kutoka katika mkataba wa silaha za nyuklia za kiwango cha kati (INF) kwa sababu Russia imekiuka mkababa huo, lakini hakutoa maelezo zaidi kuhusu uvunjifu wa mkataba huo.

Amesema Russia imekiuka mkataba huo uliosainiwa mwaka 1987 unaopiga marufuku Marekani na Russia kumiliki, kutengeneza na kujaribu kurusha makombora kutoka ardhini yenye masafa ya maili 300 hadi 3,400.

“Hatua hii ni ya hatari sana,” Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergi Ryabkov ameliambia shirika la habari la serikali ya Russia TASS Jumapili, “nina uhakika, sio tu kuwa hilo halitakubalika na jumuiya ya kimataifa lakini litasababisha kulaaniwa vikali sana.”

“Russia imekuwa ikikiuka mkataba huo. Wamekuwa wakifanya hivyo kwa miaka mingi,” Trump amesema hayo baada ya mkutano wake wa hadhara huko Elko, Nevada. “Na hatuwezi kuwaacha waendelee kwenda kinyume na mkataba huo wa nyuklia na waendelee kutengeneza silaha na sisi haturuhusiwi kufanya hivyo.”

Mkataba huo unaizuia Marekani kutengeneza silaha mpya, lakini Marekani sasa itaanza kutengeneza silaha hizo mpaka pale Russia na China watakapo kubali kuacha kumiliki au kutengeneza silaha hizo, Trump amesema. China hivi sasa hayuko katika mkataba huo.

Mnamo mwaka 2014 Rais Obama alisikitishwa na kitendo cha Urusi kuvunja makubaliano ya INF baada ya nchi hiyo kufanya jaribio la kombora moja la masafa ya kati.

XS
SM
MD
LG