Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:27

Urusi yaahidi kulipiza kisasi dhidi ya Uingereza


Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov amesema Moscow muda sio mrefu itawafukuza wanadiplomasia wa Uingereza.

Hii ni hatua ya kulipiza kisasi baada ya Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May kutangaza ana mpango wa kuwafukuza wanadiplomasia wa Urusi 23 kufuatia kitendo cha jasusi wa zamani wa Urusi kupewa sumu.

Katika kauli aliyoitoa Alhamisi Moscow, Lavrov amesema hatua alioichukua May ni ya “kijeuri” na kusema imekusudia kupoteza lengo la hali ngumu ambayo inaikabili Uingereza katika kufanya mazungumzo ya kujiondosha Umoja wa Ulaya (EU).

Lavrov amesema Moscow itaifahamisha Uingereza moja kwa moja kupitia mawasiliano rasmi kabla ya kutoa msimamo wao kwa umma.

Jasusi huyo wa zamani Sergei Skripal na binti yake, Yulia, walikutwa wamepoteza fahamu katika benchi lilioko kwenye bustani iliyoko Salisbury, huko Uingereza na kukimbizwa hospitali, ambako wako katika hali mbaya. Watu wengine kadhaa akiwemo afisa wa polisi pia wameathirika na sumu hiyo.

Uingereza imesema imejiridhisha kuwa Urusi ilihusika na shambulizi hilo la sumu na Waziri Mkuu May ametangaza kuiadhibu Urusi kwa kuchukua hatua kadhaa, ikiwemo kuwafukuza idadi kubwa kuliko yoyote ile tangu 1971 ya wanadiplomasia wa Urusi wakati wa kipindi cha vita baridi. Hata hivyo Urusi imekanusha kuhusika na shambulizi hilo la sumu.

Ikulu ya White House imetoa tamko Jumatano ikisema kuwa Marekani ina simama pamoja na mshirika wake wa karibu sana, Uingereza na inakubaliana na tathmini kuwa “Russia imehusika na shambulizi hilo la kinyama la kutumia sumu dhidi ya raia wa Uingereza na binti yake, na tunawafiki kutimuliwa kwa wanadiplomasia wa urusi na ni hatua inayostahiki.

XS
SM
MD
LG