Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 02:37

Russia inaitaka Uingereza kupunguza wafanyakazi wake Russia


Rais wa Russia, Vladimir Putin
Rais wa Russia, Vladimir Putin

Russia imeiamrisha Uingereza kupunguza zaidi ya watu 50 kutoka ofisi zake za kidiplomasia na masuala ya kiufundi huko Russia. Hayo ni madai ya karibuni kutoka Russia katika nyongeza ya ulipizaji kisasi hatua ambayo nchi zote mbili ilizifanya mwanzoni mwa mwezi huu ambapo kila nchi iliagiza kufukuzwa wanadiplomasia wengine 23.

Balozi wa Uingereza kwa Russia, Laurie Bristow
Balozi wa Uingereza kwa Russia, Laurie Bristow

Ijumaa, kremlin ilitoa agizo linalofanana kwa wanadipomasia 59 kutoka nchi 23 za magharibi katika kulipiza kisasi kwa kufukuzwa wanadiplomasia wa Russia kwenye mataifa ya magharibi. Uingereza inaonekana mlengwa kwa kuondolewa idadi kubwa ya wafanyakazi, na balozi wa Uingereza ameambiwa ana mwezi mmoja wa kupunguza wafanyakazi wake kufikia idadi sawa na wafanyakazi wa kidiplomasia wa Russia huko Uingereza.

Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya Russia kuwafukuza wanadiplomasia 60 wa Marekani na kufunga ubalozi mdogo wa St.Petersburg. Wawakilishi wa Ujerumani, Uholanzi, Ukraine, Ufaransa, Italy, Poland, Croatia, Ubelgiji, Sweden, Australia, Canada na Jamhuri ya Czech wote walionekana kuwasili katika magari ya kiofisi kwenye jengo la wizara ya mambo ya nchi za nje yaliopo kati kati ya Moscow.

XS
SM
MD
LG