Wakati wa mkutano wa asubuhi wakati wakipata istiftahi pamoja na Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg, Trump alielekeza ukosoaji wake kwa Ujerumani kwa kuruhusu kampuni ya nishati ya Ujerumani Gazprom kujenga bomba la mafuta Nord Stream 2 kupitia kwenye bahari ya nchi hiyo.
Trump aliongeza : "Kwa hiyo, ni lazima niseme ni kitu cha kusikitisha sana wakati Ujerumani inafanya makubaliano ya kiwango kikubwa cha mafuta na gesi na Russia ambapo mlitakiwa kujiepusha dhidi ya Russia. Ujerumani inafanya malipo ya mabilioni na mabilioni ya dola kwa mwaka kwa Russia. Kwa hiyo tunailinda Ujerumani, tunailinda Ufaransa, tunazilinda nchi zote hizi na baada ya hilo nchi kati hizi zinakwenda na kusaini makubaliano ya pomba la mafuta na Russia ambapo wanalipa mabilioni ya dola katika mifuko ya Russia. Lakini Ujerumani inadhibitiwa kikamilifu na Russia kwa sababu walikuwa wanapata kati ya asilimia 60 mpaka 70 za nishati yao kutoka Russia na bomba la mafuta jipya."
Wanaounga mkono ujenzi wa bomba la gesi wa dola bilioni 10 kutoka Russia wanasema unaimarisha usalama wa nishati wa nchi za Ulaya na kuongeza wigo wa biashara na inasaidia kupunguza uchafuzi wa mazingira unaotokana na moshi wa carbon dioxide.
Alipoulizwa kuhusu matamko haya ya Trump, Chansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema anajua kwa uhakika inakuwaje kuona sehemu ya Ujerumani ikimilikiwa na taifa la kigeni na hiyo siyo hali ambayo iko hivi leo.