Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 20:16

Ufaransa yafika fainali Kombe la Dunia


Samuel Umtiti akifunga goli la kichwa katika mechi dhidi ya Ubelgiji. (Foto: AP/Natacha Pisarenko)
Samuel Umtiti akifunga goli la kichwa katika mechi dhidi ya Ubelgiji. (Foto: AP/Natacha Pisarenko)

Ufaransa imeingia katika fainali ya Kombe la Dunia 2018 nchini Russia baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Ubelgiji katika mechi ya nusu fainali iliyochezwa uwanja wa St. Petersburg Jumanne.

Samuel Umtiti aliipatia Ufaransa goli la ushindi baada ya kona kutoka kwa Antoine Griezman katika dakika ya 51. Kwa mara ya kwanza katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu Ubelgiji walishindwa kupata goli katika muda wa kawaida.

Uingereza na Croatia watachuana katika mechi nyingine ya nusu fainali Jumatano katika uwanja wa Luzhniki mjini Moscow na kuamua nani atakutana na Ufaransa katika fainali ya siku ya Jumapili.

Kylian Mbappe (19) atacheza katika fainali Russia 2018
Kylian Mbappe (19) atacheza katika fainali Russia 2018

Kijana Kylian Mbappe alizidi kujizolea sifa katika mechi hiyo licha ya kuwa hakufunga goli na amejikuta katika nafasi ambayo vijana wengine wa umri wake (19) wanaota tu - kucheza katika mechi ya fainali ya Kombe la Dunia.

Ubelgiji ilitumia muda mrefu wa kipindi cha pili wakishambulia Ufaransa lakini juhudi zao zilikutana na ulinzi mkali kutoka kwa mabeki wa Ufaransa na golikipa wao.

XS
SM
MD
LG