Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 09:51

Russia yaongeza uwepo wake kijeshi barani Afrika


Rais Vladimir Putin
Rais Vladimir Putin

Russia imesema Ijumaa ina mpango wa kutuma vifaa vya kijeshi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) na kupeleka wakufunzi wa kijeshi kuyafundisha majeshi ya nchi hiyo, ikiwa inaongeza hatua muhimu ya kujihusisha kijeshi katika bara la Afrika kwa miongo kadhaa.

Russia imetoa msaada wa mamia ya silaha na kupeleka wakufunzi wa kijeshi 175 CAR mapema mwaka huu kulipa nguvu jeshi la serikali linalopambana na makundi ya wanamgambo baada ya kuondolewa vikwazo vya silaha na Umoja wa Mataifa (UN)>

Kwa mujibu wa vyanzo vya kidiplomasia na usalama, wengi kati ya Warusi waliopelekwa CAR ni walinzi binafsi wa usalama wenye mikataba na majukumu yao yameongezeka ikiwa ni pamoja na kufanya mazungumzo ya suluhu kati ya makundi hasimu yenye silaha, kutafuta miradi ya madini na kumshauri rais wa CAR.

Harakati za Russia nchini CAR ni sehemu ya msukumo wake mpana zaidi wa kurejesha ushawishi wake katika nchi za Afrika zilizoko kusini mwa jangwa la Sahara ambazo walizipoteza baada ya kumalizika Vita Baridi.

Russia imesaini makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi nan chi 19 tangu mwaka 2015 na kuongeza mahusiano ya kidiplomasia na biashara na nchi hizo.

Katika moja ya maoni mapana zaidi yaliyotolewa hivi karibuni juu ya ushirikiano huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia ametetea hatua hiyo katika tamko lake dhidi ya kile alichosema ni “wivu ‘dhahiri’” wa mataifa makubwa ya kigeni juu ya kazi inayofanywa na Russia huko CAR.

XS
SM
MD
LG