Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:25

Marekani yaitaka Russia isishirikiane na muuwaji


Shambulizi la makombora ya kemikali katika mji wa Douma nchini Syria.
Shambulizi la makombora ya kemikali katika mji wa Douma nchini Syria.

Baada ya balozi wa Russia huko Lebanon kusema kuwa majeshi ya Russia yatatungua makombora yoyote yatakayo lenga Syria, Rais wa Marekani Donald Trump amesema Jumatano kuwa Russia iwe tayari, “ kwani makombora hayo yatapigwa nchini Syria,”

“Hamtakiwi kuwa washirika wa Mnyama Anaeuwa kwa kutumia Gesi ya sumu wananchi wake wenyewe na anafurahia!” Trump amesema hayo katika ujumbe wa Twitter wakati Washington ikiendelea kupima namna ya kulishughulikia madai ya shambulizi hilo la silaha za kemikali.

Russia imesema makombora ya Marekani yanatakiwa kuwalenga “magaidi” na sio “serikali halali” ya Syria.

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov pia amesema Jumatano kuwa pande zote zinazohusika katika mgogoro wa Syria wanatakiwa kujizuilia na vitendo ambavyo vitalisambaratisha eneo hilo.

Saa kadhaa baadae, Jeshi la Russia limesema kuwa itayaweka majeshi yake huko Douma, eneo ambako shambulizi la kemikali linashukiwa kutokea Jumamosi ambalo liliuwa watu wasiopungua 40. Russia imesema majeshi yake yataendelea kuhakikisha usalama wa mji huo.

Syria imeeleza tishio la Marekani kwamba itashambulia kwa makombora kuwa ni “shinikizo la kivita lisilo na maana,” shirika la habari la serikali ya Syria limesema.

Umoja wa Mataifa na washirika wake kadhaa wameelekeza lawama kwa majeshi ya Syria kuwa yanahusika na mauaji hayo, wakati Syria na Russia wamekanusha kuwa majeshi ya Rais Bashar al-Assad yalihusika na shambulizi hilo la kemikali.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Jim Mattis amesema kuwa Marekani bado inafanya tathmini ya kintelijensia juu ya shambulizi hilo lililotokea Syria. “Tunakaa tayari kuchukua hatua za kijeshi mbalimbali iwapo zitakuwa zinaafikiana na maamuzi ya rais,” amesema Jumatano.

XS
SM
MD
LG