Miongoni mwa unyanyasaji ulotajwa ni pamoja na mauaji, mateso na kukamatwa kiholela kwa watu hao.
Ripoti ya kila mwaka iliyotolewa na Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres imetaja pia kuwepo na kampeni kuwafuatilia, kuwatendea maovu, na kuwaaibisha hadharani watetezi wa haki za binadam na waathiriwa.
Mataifa hayo 38 yanajumuisha 29 yenye kesi mpya na mengine 19 yakikabiliwa na kesi zinazoendelea.
Ripoti inaeleza kwamba mataifa mengi yanadaiwa kuwafungulia mashtaka wanaharakati wa haki za binadamu kwa ugaidi au kushirikiana na mataifa ya kigeni kuhujumu hadhi na usalama wa taifa, ikiwa ni njia ya kuwatishia wasiendelee kushirikiana na UN katika uchunguzi huo.
Kesi hizo mpya zinazochunguzwa ziko Bahrain, Cameroon, China, Colombia, Cuba, DRC, Djibouti, Misri, Guatemala, Guyana, Honduras, Hungary, India Israel, Krygyszstan, Maldives.
Nyingine ni Mali Morocco, Myanmar. Ufilipino, Rwanda. Saudia Arabia, Sudan Kusini, Thailand, Trinidad na Tobago, Uturuki, Turkmeni na Venezuela.