Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 04:50

Shambulizi la kutumia kisu lajeruhi watoto 14 China


Eneo la Chongqing, China
Eneo la Chongqing, China

Mwanamke mmoja aliyekuwa amebeba kisu aliwashambulia wanafunzi wa shule ya chekechea magharibi ya China Ijumaa asubuhi, na kuwajeruhi watoto 14.

Mshambuliaji huyo, aliyetambuliwa kwa jina lake la familia Liu, aliwashambulia watoto hao wakati wakirejea shuleni katika jiji la Chongqing baada ya mazoezi yao ya viungo asubuhi. Wanafunzi wote walipelekwa hospitali.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 39 alipelekwa na kuwekwa rumande polisi.

China imewahi kuwa na mashambulizi ya namna hii katika miaka ya karibuni. Mashambulizi hayo yamekuwa mara nyingi yakilaumu hali ya afya ya akili ya watu hao au mtu ambaye ana chuki.

China ina sheria inayo kataza kuuza au kumiliki silaha za moto. Mashambulizi kama haya yanayo elekezwa kwa watu wengi kwa kawaida yanafanywa kwa kutumia visu na mabomu yaliyo tengenezwa kienyeji.

XS
SM
MD
LG