Nchi ambazo zinadai kuwa na haki eneo la bahari ambapo meli zinafanya safari zake wakati ndege za Washington zikiendelea kuzuia harakati zozote za kuongeza shughuli za baharini zinazo fanywa na China ambaye ana pinga uwepo Marekani katika eneo hilo.
Wachambuzi wana amini ndege hizo za kivita aina ya B-52 zinazoruka katika eneo, kwa kipindi cha miezi miwili iliyopita, itaipa Brunei, Malaysia, Ufilipino na Vietnam namna fulani ya ulinzi dhidi ya Beijing. Nchi hizo pia zinaweka shinikizo kuwepo uhuru wa kutumia eneo hilo la bahari ya South China lililo na rasilmali nyingi.
Ndege ya kivita ya Stratofortress “ilifanya operesheni zake” katika Bahari ya South China na Bahari ya Hindi Septemba 23 na 25, kikosi hicho cha anga cha Pacific cha jeshi la Marekani kimesema katika tamko lake wiki iliyopita. Ndege aina ya B-52 iliruka kutoka Guam katika “zoezi la mafunzo la kawaida,” tamko hilo limesema.
Madai ya Nchi za Kusini mashariki mwa Asia ni kuwa nchi zote zinapaswa kuhamasika na zeozi hili la ndege zinazoruka katika eneo hilo, ambazo zinaonyesha nia yake ya kudhibiti vitendo vya China katika eneo hilo,” amesema Yun Sun, mtafiti wa ngazi ya juu katika Programu ya Mashariki ya Asia kwenye kituo cha utafiti cha Stimson, Washington.
Jeshi la China limepinga hatua hiyo ya Marekani kurusha ndege zake za kivita na kukiita “ ni kitendo cha uchokozi” na kutaka hatua zichukuliwe.