Ndege hiyo ilikuwa inaelekea mji wa Pangkal-Pinang nchini indonesia.
Yusuf Latif, msemaji wa idara ya huduma za uokoaji na kuwatafuta manusura wa ajali hiyo, amewaambia wanahabari kuwa Imethibitishwa ndege hiyo imeanguka.
Naye msemaji wa shirika hilo la ndege Sutopo Purwo amewaambia waandishi wa habari kwamba kati ya waliokuwa ndani ya ndege hiyo aina ya Boeing 737 MAX, JT610 ni watoto watatu na wafanyakazi wa shirika hilo la ndege 7.
Ajali hiyo ni ya kwanza kuhusisha ndege ya Boeing 737MAX ambayo imeuzwa sana kote duniani kutokana na injini yake kutumia kiwango kidogo cha mafuta.
Kwa mujibu wa Waziri wa Fedha wa Indonesia kulikuwa na maafisa 20 wa wizara hiyo ndani ya ndege waliokuwa wakirudi kazini Pangkal Pinang baada ya kutembelea familia zao mjini Jakarta.