Maafisa wa Uturuki wanasema kuwa mwandishi huyu aliuwawa na mwili wake kukatwa katwa na majasusi wa Saudi Arabia ndani ya ubalozi wa Riyadh mjini Istanbul, tuhuma ambazo Saudia inakanusha.
Wakati akielekea Ankara kufanya mazungumzo na viongozi wa Uturuki juu ya uchunguzi unaohusu kutoweka kwa mwandishi Jamal Khashoggi, mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Marekani amewaambia waandishi kuwa Mfalme Salman na Prince Mohammed bin Salman amemhakikishia kuwa “watawafahamisha watu dunia nzima” matokeo ya uchunguzi wao.
Pompeo amesema Saudia imeahidi kumwajibisha “mtu yoyote aliyehusika na kutenda kosa lolote litakalo gundulika katika uchunguzi huo,” bila ya kumwacha yoyote anayehusika na mauaji hayo, hata ikiwa ni wanafamilia wa Ufalme wa Saudia.
Lakini alipoulizwa iwapo maafisa wa Saudia wamemfahamisha iwapo Khashoggi yuhai au amekufa, Pompeo amesema, “Sitaki kuzungumzia masuala yoyote yanayo fahamika juu ya mwandishi. Utawala wa Saudia pia hautaki kuzungumzia hilo, wanataka wapewe muda wa kukamilisha uchunguzi huu kikamilifu.