Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 03:24

WFP yasema mamilioni ya watu wanalala na njaa kutokana na vita


Balaa la njaa katika mabara ya Afrika na Asia
Balaa la njaa katika mabara ya Afrika na Asia

Shirika la Chakula Duniani (WFP) limetahadharisha kuwa mamilioni ya watu duniani wanalala na njaa kwa sababu gharama za kuwapatia chakula zimeendelea kupanda kutokana na migogoro, na matatizo mengine ya dharura.

Katika ripoti ya WFP 2017 iliyotolewa hivi karibuni, imeeleza mahitaji ya kibinadamu na matatizo ya dharura ya ulimwenguni yanaendelea kuongezeka, kama ilivyokuwa kwa gharama za kuwapatia chakula wale wenye njaa.

Msemaji wa WFP Bettina Luescher amesema yapata watu milioni 800 duniani ambao wanakabiliwa na njaa.

Amesema kuwa wengi wao wanajikuta wako katika migogoro ya kivita na maafa ya kawaida. Wengine, amesema, kimya kimya wanaangamia kwa kutokuwepo vyombo vya habari na matangazo yanayohitajika kupasha habari juu ya matatizo yao.

“Tunajua namna ya kumaliza njaa, lakini juhudi zetu zote zinagonga ukuta, pingamizi au kuzuiliwa kwa sababu ya migogoro ya kivita inayoendelea. Na, hilo kwangu ni aina fulani ya janga kubwa,” Luescher amesema.

Shirika la WFP limeripoti kuwa gharama ya kutoa chakula cha msaada imeongezeka kwa zaidi ya asilimia 140 kutoka dola za Kimarekani bilioni 2.2 mwaka 2009 kufikia dola bilioni 5.3 mwaka 2015. Luescher amesema kiwango cha fedha kinachohitajika kwa ajili ya programu ya misaada ya kibinadamu mwaka huu inategemewa kuongezeka kwa zaidi ya dola za Kimarekani bilioni 9.

WFP imeripoti kuwa maeneo mawili – upande wa mashariki na kati ya Afrika na Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini- zinagharimu asilimia 70 ya matumizi ya WFP. Inasema kuwa takriban moja ya tatu ya bajeti yake inatumika katika misaada ya kibindamu kwa nchi nne zinazopambana kutokomeza njaa – Nigeria, Somalia, Sudan Kusini na Yemen.

XS
SM
MD
LG