Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 16:18

Idadi ya waliokufa katika maporomoko ya ardhi DRC yafikia 150


Ramani ya Tanzania
Ramani ya Tanzania

Idadi ya vifo kutokana na maporomoko ya ardhi ambayo yamekikumba kijiji kimoja cha uvuvi kwenye kingo la ziwa huko jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imefikia 150.

Kwa mujibu wa shirika la habari la ufaransa, kiongozi wa serikali ya Congo amesema Jumatatu serikali inakadiria kwamba kuna miili kiasi cha 100 imefukiwa chini ya mawe makubwa ambayo yalianguka na kuharibu nyumba 48.

Kwa upande wake naibu Gavana wa jimbo la ituri, pacifique Keta amesema, maporomoko ya ardhi yalitokea jumatano iliyopita katika kijiji cha kaskazini mashariki cha Tora kwenye ukingo wa ziwa Albert.

Maafa hayo yalitokea wakati sehemu ya mlima ulipofunika sehemu ya kambi ya uvuvi baada ya mvua kubwa kunyesha. Serikali imesema hakuna matumaini ya kupata miili ya wale waliofunikwa na matope.

Pia taarifa kutoka katika eneo hilo zinasema kuwa kumekuweko na harufu za miili iliyooza ambayo imeenea katika eneo hilo la tukio na tayari kuna juhudi za kuwahamisha wakazi wa eneo hilo kuhama ili kuwaepusha na maamubikizi ya ugonjwa wa kipindupindu.

XS
SM
MD
LG