Hatuna matatizo kufanya mazungumzo na upande mwengine. Tutafanya tathmini na kuamua iwapo mazungumzo ya Stockholm yanapewa umuhimu unaotakiwa au la kesho,” msemaji wa waasi ameuambia mtandao wa televisheni ya lugha ya Kiarabu.
Wawakilishi wa serikali ya Yemen na wale wa waasi wa Houthi, pande mbili ambazo zimekuwa katika vita nchini humo, wamelaumiana vikali katika kikao cha kwanza cha mazungumzo ya kutafuta amani ambayo Marekani imeeleza ni magumu lakini muhimu sana.
Mazungumzo ya Sweden ni ya kwanza katika kipindi cha miaka miwili, kufuatia vita vya uharibifu kati ya muungano wa wanajeshi wa Saudi Arabia wanaounga mkono serikali na waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran.
Mapigano yamesababisha ukosefu mkubwa wa chakula nchini Yemen, na Umoja wa mataifa umeeleza wasiwasi mkubwa wa kuzuka njaa nchini humo.
Hata hivyo upande wa waakilishi wa serikali na wa waasi walikuwa wamekubaliana kubadilishana wafungwa na kuondoa wapiganaji walio jeruhiwa kutoka sehemu ya vita ili wapate matibabu mjini Oman, kabla ya mazungumzo, pande zote zimejikita katika kutaka matakwa yake yatekelezwe wakati wa kikao.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, ametaka pande husika kutowekeana masharti huku upande wa waasi ukisema kwamba ulikuwa bado unathathmini uzito wa mazungumzo hayo.
Maungumzo hayo katika kijiji cha Rimbo, kaskazini mwa Stockholm, yanayo wafanya washiriki kula meza moja, yataendelea kwa muda wa wiki moja.