Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 12:16

Mvutano wa Marekani na Iran unatishia kuingilia kati mkutano wa tabia nchi UN


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres

Wakati viongozi wa dunia wakijitayarisha kukutana katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) wa kila mwaka, hali ya mvutano inaendelea kuongezeka kati ya Marekani na Iran kukiwa na wasiwasi mvutano huo utagubika kilele cha mazungumzo ya kuongezeka joto duniani.

“Tukubali kukabiliana na hili, hatuna nafasi ya kupoteza fursa hii. Tunajikosesha kuungana kudhibiti mabadiliko ya tabia nchi,” Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewaambia waandishi Jumatano.

“Ulazima wa kuchukuwa hatua hauwezi kuwa wazi zaidi ya hivi, na ndiyo maana nimeitisha mkutano huu wa kutafuta suluhisho la mabadiliko ya tabia nchi.”

Mvutano kati ya Marekani na Iran unaweza kuziba fursa

Kilele cha mkutano huo kitafanyika Jumatatu, na zaidi ya viongozi 100 wa nchi mbalimbali na serikali wanatarajiwa kuhudhuria. Ni wale tu ambao wataleta msukumo na mipango Madhubuti ambayo itasaidia kukabiliana na athari za kuongezeka kwa joto duniani watakaribishwa kuongea katika mkutano huo.

Guterres, ambaye amefanya suala la kimkakati ni kudhibiti kuongezeka kwa mabadiliko ya tabia nchi, amesema anatarajia kuwepo “mipango muhimu” itakayo saidia kwa kiwango kikubwa kupunguza uchafuzi wa mazingira katika kipindi cha muongo unaokuja na kufikia kutokuwepo hewa chafu ya carbon ifikapo 2050.

“Tutaonyesha juhudi zenye tija zinazokusudia kuondokana na matumizi ya makaa ya mawe, kutoa motisha wa fedha kwa kutozalisha gesi chafu, kuacha kutoa ruzuku kwa uzalishaji wa makaa ya mawe, na kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa unaoathiri afya zetu,” amesema.

“Pia tutaweka mkazo juu ya umuhimu wa kuongeza utatuzi wa uharibifu wa mazingira kutumia vitu asilia, kutengeneza utaratibu salama katika mazingira ya kazi na shughuli za kijamii, kujenga uhimilivu, kuwalinda watu, kukusanya fedha na kushawishi ajira salama katika hatua hii ya mpito."

UN inataka kuendeleza maamuzi yaliyofikiwa katika makubaliano ya mkutano wa hali ya hewa wa Paris 2015 yenye lengo la kudhibiti kuongezeka kwa joto duniani katika karne hii kufikia nyuzi joto 2 juu ya kiwango kilichokuwa kabla ya kuanza viwanda.

XS
SM
MD
LG