Mkutano huo wiki hii unafanyika mjini Katowice na unakabiliwa na changamoto kubwa ya kuziunganisha nchi za dunia kukubaliana juu ya namna ya kutekeleza makubaliano ya kihistoria ya Paris ya 2015, yanayobidi kuanza 2020 juu ya kupunguza joto la dunia kwa nyuzi 1.5 celsus.
Waatalamu wanasema wanahofu kwamba mataifa yameanza kurudi nyuma katika utekelezaji wa makubaliano hayo amabyo wanasema yanahitaji mataifa makuu tajiri kugharimia sehemu kubwa ya miradi ya kulinda mazingira ambapo mataifa maskini ndiyo yataathirika zaidi pindi malengo hayo hayajatekelezwa.
Mazungumzo yalipoanza huko Poland, maelfu ya watu walijitokeza katika mji mkuu wa Ubelgiji wa Brussels kuandamana kuzitaka nchi za dunia kuchukua hatua za dhati za kupunguza kuongezeka kwa joto dunianiu na kuloinda mazingira.