Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 11:48

Wanafunzi Australia, New Zealand washinikiza wanasiasa, wafanyabiashara kuchukuwa hatua


FILE - Vijana wasema katika ujumbe wao kuwa "ulafi wa kupata faida unaangamiza dunia" wakati wa maandamano ya wanaharakati wa "Fridays For Future" ukitaka viongozi wachukue hatua kulinda mazingira Machi 15, 2019, huko Berlin.
FILE - Vijana wasema katika ujumbe wao kuwa "ulafi wa kupata faida unaangamiza dunia" wakati wa maandamano ya wanaharakati wa "Fridays For Future" ukitaka viongozi wachukue hatua kulinda mazingira Machi 15, 2019, huko Berlin.

Maelfu ya wanafunzi nchini Australia na New Zealand wameandamana Ijumaa wakianzisha siku ya kimataifa kupinga hali ya kutokuwepo hatua yoyote kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Waandaaji wa maandamano hayo wanatarajia kuwa zaidi ya vijana milioni moja katika majimbo 120 katika nchi hizo watashiriki katika maandamano hayo.

Waandamanaji hao wanashinikiza kwamba viongozi wa kisiasa na kibiashara wachukuwe hatua za mara moja kupunguza kuongezeka kwa joto duniani kutokana na moshi wa gesi huo viwandani kuendelea kuharibu mazingira duniani.

Wanafunzi huko Frankfurt, Ujerumani waliandamana kuelekea makao makuu ya Benki Kuu ya Umoja wa Ulaya (ECB) kuishinikiza iache kufadhili viwanda vya mafuta venye kuleta uchafuzi wa hali ya hewa.

Kwa mujibu wa wanasayansi wa mazingira, gesi za viwandani zinazotokana na mafuta yanayounguzwa na kutoa moshi vimesababisha ukame na joto kali, ikiyayusha theluji, na kusababisha kina cha bahari kuongezeka na mafuriko yenye uharibifu.

Maandamano ya kupinga uharibifu wa tabia nchi yalianzishwa na Greta Thunberg, mwanaharakati wa Sweden mwenye umri wa miaka 16, aliyeanza peke yake kupinga uharibifu wa mazingira nje ya bunge la Sweden Agosti. Tangu wakati huo shule ya msichana huyo ilioanzisha harakati za kupinga uharibifu huo zinazojulikana kama “The Fridays for Future” (Ijumaa iliyotengwa kwa ajili ya mustakbali wa dunia” umekua kwa kasi kubwa.

Moshi wa Carbon duniani umefikia rikodi ya juu mwaka 2018, pamoja na kuwepo onyo kutoka Jopo la Muungano wa serikali juu ya Mabadiliko ya Tabia Nchi unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa lililotolewa Octoba kuwa moshi wa gesi chafu lazima uzuiliwe kwa kipindi cha miaka 12 ijayo ili kuimarisha hali ya mazingira.

XS
SM
MD
LG