Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 23:23

Tanzania yasisitiza ushirikiano kufikia matumizi endelevu ya mto Nile


Mto Nile
Mto Nile

Mawaziri wa maji wa nchi kumi wananchama zilizoko kwenye mtiririko wa bonde la mto Nile hususan za maziwa makuu (NELCOM) wameanza mkutano wa 21 wa siku mbili jijini Dar es Salaaam, Tanzania, unaolenga, pamoja na mambo mengine, ,kujadili matumizi sawa ya rasilmali ya maji katika mto huo.

Wakati huohuo serikali ya Tanzania imeendelea kusisitiza iko fursa ya kupatikana muwafaka juu ya migogoro inayosababishwa na matumizi ya maji ya mto huo pamoja na Ziwa Victoria .

Akifungua mkutano huo Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, ameeleza kuchoshwa na mijadala kama hiyo isiyo kwisha na kutoa wito kwa nchi hizo kumi zinazo tumia maji ya mto Nile kufikia muwafaka wa kuviondoa vikwazo vikuu viwili ambavyo ni kutoundwa kwa kamisheni ya bonde hilo, na wanachama kutotoa kwa wakati michango ya taasisi inayo simamia wanachama wake inayo julikana kwa kifupi NBI.

Tanzania yahimiza ushirikiano

Waziri Mkuu amesema nchi wanachama hazina budi kuimarisha ushirikiano wake. Amesema Waswahili tunaomsemo wetu maarufu : “Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu.”

Majaliwa amesisitiza kuwa bila ya ushirikiano “ hatuwezi kusimamia matumizi endelevu ya maji. Bila ya ushirikiano hatuwezi kushughulikia changamoto zinazo zikabili bonde letu.”

Ameongeza kuwa changamoto kubwa ilioko hivi sasa ni kupungua kwa mtiririko wa maji kwenda Ziwa Victoria ambayo ni moja ya vyanzo muhimu vya mto Nile.

“Kupungua huko kwa maji kumetokana na uharibifu wa mazingira, kando kando ya mto Nile, lakini pia mabadiliko ya tabia nchi. Hivyo basi mmbuni kushirikiana katika kukabiliana na changamoto hizo kwa pamoja,” amefafanua.

Majaliwa amesisitiza kuwa kuendelea kuwepo kwa mto Nile kutategemea kuwepo ushirikiano “wetu “vilevile.

Pia amesisitiza kuwa kutokuwepo kwa mto Nile kunategemea kudharau haya ambayo nimeyatamka hapa.

“Hatuna budi kuongeza utashi wa kisiasa katika kutekeleza miradi ya pamoja,” amesema.

Tuchukulie hii ni fursa

Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Dkt Augustine Mahiga ametaka matumizi ya bonde la mto Nile na ziwa vctoria iwe kama fursa za kuleta maendeleo na sio chuki miongoni mwa wanachama.

“Hakutakuwa na vita wala ushindani kati yetu, kwa sababu tunakaa na kuzungumza matatizo yatokanayo na matumizi ya maji na ndio maana tuko hapa leo,” ameeleza.

Mahiga anasema matatizo hayawezi kukosekana katika matumizi ya mto Nile.

“Tunajenga mabwawa, iko Aswan Dam kule Misri, na mabwawa mengine. Linajengwa bwawa kule Ethiopia, ambalo litatoa megawati zaidi ya 6,000. Kuna mabwawa Uganda, kuna mabwawa Tanzania na kuna mabwawa Sudan.

Waziri Mahiga asema sasa haya yataleta changamoto, sasa change moto hizi sasa hatutaki ziwe chanzo cha migogoro, chanzo cha ugomvi.

“Nataka iwe ni fursa ya kushirikiana na ndio maana tuko hapa,” amehimiza Mahiga.

XS
SM
MD
LG