Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 23:21

Rais wa Misri yuko tayari kutatua mzozo wa mto Nile


Rais Abdel-Fattah el-Sissi
Rais Abdel-Fattah el-Sissi

Misri imesema inafanya kila linalowezekana kutatua mzozo wa matumizi ya mto Nile na mataifa washiriki.

Balozi wa Misri nchini Rwanda Namira Negm amesema hayo mjini Kigali baada ya rais wa Misri Abdul Fatteh El Sissi kuanza ziara yake ya siku mbili nchini humo.

Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili VOA ameripoti kuwa Rais Abdul Fatteh el Sissi amewasili mjini Kigali mapema Jumatano akiambatana na baadhi ya viongozi waandamizi kwenye serikali yake.

Alipokelewa kwenye uwanja wa ndege wa Kigali na Rais Paul Kagame kabla ya kuelekea moja kwa moja kwenye jumba la makumbusho la mauaji ya kimbari.

Baadaye jioni Jumanne Rais huyo wa Misri anatazamiwa kupokelewa kwa karamu maalum kabla ya kusaini makubaliano ya kiuchumi baina ya Misri na Rwanda.

Balozi wa Misri nchini Rwanda Namira Negm amesema pia kiini cha ziara ya Rais huyo nchini Rwanda ni kujaribu kufufua mafungamano ya Misri na nchi nyingine za Kiafrika.

“Chini ya Uongozi wa Rais Sissi tunajaribu kujeresha uhusiano uliokuwepo tangu enzi ya ndugu zetu waafrika, hususan nchi za bonde la mto Nile.

Nadhani maazimio yaliyochukuliwa mjini Entebbe yatakuwa ni sehemu ya Rais Sissi na Rais Kagame, na lakini kimsingi tutatazama mzozo baina ya Misri na baadhi ya mataifa mengine, ili kuona jinsi tunavyoweza kutatua utata huu kwa sababu tunahitaji ushirikiano badala ya migogoro.

Misri imekuwa na mzozo wa miongo mingi hasa kuhusu umiliki na matumizi ya mto Nile.

Rais Abdul Fatteh El Sissi ayatembelea mataifa manne ya mashariki na magharibi mwa Afrika.

Balozi Namira Negm anasema, “mataifa haya yana ushawishi mkubwa kuhusu suala hilo akitoa mfano wa Rwanda muhimu sana kuihusisha Rwanda kwenye majadiliano haya ambayo ni lazima yaende sambamba na sheria za kimataifa.”

Kwa upande mwingine wafanyabaishara wa Rwanda wanaichukulia zaidi ziara hii kama nafasi muhimu ya kufungua ukurasa wa mawasiliano ya kibiashara baina yao na wenzao wa Misri.

XS
SM
MD
LG