Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 00:27

Wasichana katika maeneo ya Ziwa Victoria bado wako nyuma kielimu


Wanafunzi wasichana wakitembea kwenda shule huko Imbirikani, Kenya. April 2016.
Wanafunzi wasichana wakitembea kwenda shule huko Imbirikani, Kenya. April 2016.

Maeneo hayo mara nyingi yanakumbana na changamoto zinazotokana na umaskini ambao kwa kiasi kikubwa umeendelea kuathiri maendeleo ya kiuchumi.

Katika maeneo yaliyoko pembezoni mwa ziwa Victoria, watoto wa kike bado wanakabiliwa na kiwango duni cha elimu, kinyume na takwimu za Serikali ya Kenya.

Mwandishi wa VOA Kennedy Wandera amesema kuwa katika eneo la Bunyala Magharibi nchini humo, wasichana wengi wameacha kwenda shule baada ya kupata uja uzito na vile vile kujiingiza katika ndoa za utotoni.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Wizara ya Elimu kiwango cha elimu kwa wanafunzi wa kike nchini Kenya kwa ujumla kimeonyesha kuimarika zaidi kuliko kile cha wanafunzi wanaume.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:06 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Alipokuwa akitembelea maeneo hayo hivi karibuni amesema hali hii ya wanafunzi hawa kielimu kuwa nyuma ni sababu ya vitendo hasi vya wazazi na jamii vinavyo kwamisha juhudi za serikali kuendeleza elimu nchini Kenya.

Patrick Okello ambaye ni mwalimu wa Bridge International Academies katika eneo la Bunyala Magharibi ameiambia VOA kuwa masomo hayajapewa kipaumbele katika maeneo haya ya magharibi na badala yake uvuvi ndio umetia kasi.

Okello ameshauri kuwa wazazi wanapaswa kuhamasishwa na kuelezwa ubora wa elimu ili kuliinua eneo hilo kielimu.

“Tunawatembelea wazazi nyumba hadi nyumba kujaribu kuwaelezea umuhimu wa elimu,” alisema.

Hata hivyo maeneo mengine hususan yale yanayopakana na Ziwa Victoria yameripotiwa kusajili idadi ndogo mno ya wanafunzi wa kike.

Maeneo hayo mara nyingi yanakumbana na changamoto zinazotokana na umaskini ambao kwa kiasi kikubwa umeendelea kuathiri maendeleo ya kiuchumi.

Lakini kile kinachoshtusha ni kushuka kwa elimu ya mtoto wa kike. Eneo la Mau Mau, Bunyala katika kaunti ya Busia ni mojawapo ya maeneo ambayo elimu ya mtoto wa kike imedidimia kabisa amesema Collette Nerima, mwalimu wa Bridge International Academies.

Bridge International Academies ni mojawapo ya mashirika ya kigeni nchini Kenya yanayotoa elimu katika shule za chekechea pamoja na za msingi.

XS
SM
MD
LG