Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 16:45

Maandamano nchi 95 yahimiza makaa ya mawe kutotumika


Meli inayo peperusha mabango zikiingia katika bandari ya Sydney, Australia, Septemba 8, 2018.
Meli inayo peperusha mabango zikiingia katika bandari ya Sydney, Australia, Septemba 8, 2018.

Meli zinazo peperusha mabango yanayo tahadharisha mabadiliko ya tabia nchi na kutaka hatua zichukuliwe zimeingia katika bandari ya Sydney nchini Australia, ikianzisha wimbi jipya la maandamano katika nchi 95 kote duniani.

Maandamano hayo yameandaliwa na kikundi kinachopigania mazingira Lobby group 350.org kilichoko New York.

Ujumbe huo kutoka kwa wanaopigania usalama wa mazingira uliofikishwa katika bandari ya Sydney umepokelewa katika miji midogo na mikubwa duniani kote, wakati wafanya kampeni dhidi ya uharibifu wa mazingira wakitaka makaa ya mawe yasitumika kamwe.

Australia imeendelea kuwa inategemea sana makaa ya mawe kuzalisha umeme, lakini wanaharakati wanaotaka mazingira yalindwe wanasema lazima iungane na juhudi za kimataifa katika kutafuta nishati mbadala endelevu.

Serikali huko Canberra, imefuta mpango wa nishati wa kitaifa ambao ungepunguza uchafuzi wa mazingira na kuboresha sekta salama ya nishati, na baadhi ya wabunge wanataka Australia kujiondoa kutoka katika mkataba wa mazingira wa Paris kwa sababu ya athari ya viwanda vinavyotumia nishati yenye kuchafua mazingira.

Wiki hii Australia na New Zealand ziliungana na nchi zilizoko katika bahari ya Pacific na kwa pamoja zimetangaza kuwa mabadiliko ya tabia nchi ndiyo “tishio kubwa pekee” kwa mataifa hayo ambayo ni visiwa katika eneo hilo.

“Nchi za Pacific zina niya ya dhati kushikamana na Mkataba wa Paris, kwa sababu ni msingi wa kuendelea kwa visiwa hivyo kuwepo katika bahari ya Pacific,” amesema Dame Meg Taylor, katibu mkuu wa Jukwaa la Visiwa vya Pacific.

Viongozi wa eneo wanasema kuwa mabadiliko ya tabia nchi tayari yamekuwa na athari kwa eneo hilo ikiwemo kuongezeka kwa kina cha bahari kinacholeta mmomonyoko waardhi na mawimbi yenye nguvu yanayo sababisha mafuriko katika visiwa hivyo.

XS
SM
MD
LG