Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 14:49

Museveni azilaumu Kenya na Tanzania kwa uchafuzi wa Victoria


Rais Yoweri Museveni wa Uganda
Rais Yoweri Museveni wa Uganda

Pia ametaja uchafuzi wa mazingira katika mito kadhaa katika nchi za Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Tanzania na Uganda kutokana na matumizi ya rais yasiyozingatia utunzaji wa mazingira.

Kadhaalika ameelezea masikitiko yake juu ya uchafuzi na uvamizi wa ardhi zenye rutuba akisema ndiyo kichocheo hasa cha ukame unaoshuhudiwa hivi sasa katika nchi hizi.

FILE - Wavuvi katika Ziwa Victoria nchini Uganda, Nov. 3, 2006.
FILE - Wavuvi katika Ziwa Victoria nchini Uganda, Nov. 3, 2006.

​Wakati huo huo mwandishi wa idhaa ya Kiswahili VOA amesema nchi za kiafrika zimetakiwa kuungana sio tu kwa maslahi ya kibiashara lakini kiulinzi pia kile ambacho kimeelezewa kuwa ni uchokozi wa nchi zenye nguvu duniani.

Rais Yoweri Museveni wa Uganda Jumanne amesema hayo huku akizitaka nchi za Afrika Mashariki kupitisha sheria itakayozuia ununuzi wa bidhaa kutoka nje na kuzilazimisha nchi zinazotaka kufanya biashara Afrika Mashariki kuanzisha viwanda ndani ya jumuiya hiyo.

Ameripoti kuwa Museveni alikuwa akihutubia wabunge wa jumuiya ya afrika mashariki wakati wa ufunguzi wa kikao chao cha awamu ya nne.

Amesema kuwa Museveni amesema kuwa wakati umefika kwa bara la Afrika kuwa na muungano utakaowezesha nchi hizo kujilinda kiusalama na kujihami kivita.

Kwa mujibu wa Museveni jinsi bara la Afrika lilivyo hivi sasa kuna uwezekano wa kuvamiwa na nchi yoyote na kuyumbishwa kiuchumi pamoja na kiusalama. Ametaka nchi za Afrika kujifunza kutoka nchi alizoziita ndogo ambazo zinalindwa na nchi kubwa.

Museveni pia amesema kwamba wakati umefika kwa nchi za Afrika mashariki kuzilazimisha nchi zilizoendelea kuwekeza katika viwanda ndani ya jumuiya hii kwani Afrika Mashariki inapoteza kiasi kikubwa cha pesa kwa kuagiza bidhaa nje.

Kwa mfano Museveni ametaka hatua za haraka zichukuliwe kupiga marufuku uagizaji wa nguo ili kufufua viwanda vya kutengeneza nguo pamoja na kuimarisha kilimo cha pamba, akisema “tunaweza kuiga mfano wa Ethiopia.”

Akitoa mfano wa Tanzania na Kenya, Museveni amesema Afrika mashariki ina miundo mbinu ya kutosha kama barabara za kisasa, pamoja na amani ya kudumu kwa wawekezaji na kwamba haoni sababu za nchi za Afrika mashariki kuendele kuagiza bidhaa kutoka nje ya Afrika.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Kennes Bwire, Uganda

XS
SM
MD
LG