Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 12:34

Athari za Kimbunga Idai : Msumbiji yathibitisha mlipuko wa kwanza wa kipindupindu


António Guterres
António Guterres

Serikali ya Msumbiji na mashirika ya misaada ya kimataifa wakati wakiendelea kujitahidi kukabiliana na uharibifu mkubwa na pia tatizo la watu kukosa makazi baada ya kimbunga Idai kupiga Mozambique sasa kuna janga jipya la ugonjwa wa kipindupindu nchini humo.

Afisa wa ngazi ya juu Ussene Isse amewaambia waandishi wa habari Jumatano kuwa kuna watu watano waliopata mambukizi ya kipindupindu waliogundulika katika eneo jirani na pwani ya Jiji la Beira, ambalo lilikumbwa na uharibifu mkubwa wakati mafuriko hayo yalipotokea Msumbiji, Malawi na Zimbabwe mwisho wa wiki iliyopita.

Mvua hiyo iliharibu miundombinu ya mji huo, ikiwemo mfumo wa usambazaji maji safi na taka.

Kipindupindu ni ugonjwa unaoambukizwa na vijidudu ambavyo kwa kawaida vinamuathiri mwandamu anapokunywa maji yaliyo hatarishi na pia mazingira machafu, na hupelekea mtu kupata ugonjwa wa kuharisha sana ambao unaweza kumuua mtu katika kipindi cha masaa kadhaa iwapo hatapata matibabu.

Wafanyakazi wa afya pia wanakabiliana na idadi inayoongezeka ya watu ambao wanasumbuliwa na hali mbaya ya kuharisha maji. Shirika la Afya duniani linasema chanjo za kipindupindu 900,000 za kunywa zinatarajiwa kuwasili katika eneo hilo wiki hii.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema Jumanne kuwa jumuiya ya kimataifa inatakiwa kuchukua hatua za haraka kuchangia katika kuzisaidia nchi tatu za kusini mwa Africa ambazo zimeathiriwa vibaya sana na kimbunga Idai.

XS
SM
MD
LG