Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 23:17

Kimbunga Idai : Wahanga Msumbiji, Malawi, Zimbabwe huenda wakafikia 1000


Mafuriko na uharibifu uliletwa na kimbunga Idai, Beira, Mozambique, Machi 17, 2019
Mafuriko na uharibifu uliletwa na kimbunga Idai, Beira, Mozambique, Machi 17, 2019

Idadi ya watu waliokufa kutokana na kimbunga Idai nchini Msumbiji, Malawi na Zimbabwe, huenda ikafikia watu 1000.

Haya yameelezwa na Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi, aliyenukuliwa na radio inayomilikiwa na serikali ya Msumbiji.

Zaidi ya watu 150 wamethibitihswa kufa na mamia hawajulikani walipo kufuatia kimbunga Idai, kilichopiga kusini mashariki mwa Afrika, mji wa Beira, nchini Msumbiji ukiwa umeharibika kabisa.

Timu ya uokoaji wakiwemo wafanyakazi wa Shirika la Msalaba Mwekundu imewasili katika mji wa Beira kuweza kutathmini kiwango cha uharibifu.

Jamie Le Sueur, anayeongoza timu hiyo, ametaja kuwa hali ni mbaya sana, akieleza uharibifu mkubwa uliyosababishwa na kimbunga hicho na kuongezea kwamba asilimia 90 ya sehemu iliyokumbwa na janga hilo, imeharibika kabisa.

Umoja wa mataifa unakadiria kwamba zaidi ya watu milioni 1.5 wa Msumbiji, Malawi na Zimbabwe wameathirika na dhoruba hiyo. Serikali ya nchi hiyo imetangaza hali ya dharura nchini Zimbabwe.

Kimbunga Idai, kilipiga pwani ya Beira, Msumbiji, Alhamisi wiki iliyopita, kikiwa na upepo uliovuma kwa kasi ya kilomita 200 kwa saa, kabla ya kuelekea magharibi katika nchi za Malawi na Zimbabwe.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG