Shirika hilo limeposti ujumbe wa Twitter kuwa ndege hiyo nambari 302 iliruka majira ya saa 8:38 asubuhi kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole na kupoteza mawasiliano saa 8:44.
Ujumbe huo umeongeza kuwa juhudi za kuitafuta ndege hiyo na ukoaji zinaendelea na hadi sasa hakuna taarifa yeyote juu ya abiria na wafanyakazi hao waliokuwa ndani ya ndege hiyo.
Waziri Mkuu Abiy Ahmed amesema katika ujumbe wake wa Twitter : “Ofisi ya Waziri Mkuu, kwa niaba ya serikali na watu wa Ethiopia, wanatoa rambirambi zao kwa familia za watu wote waliopoteza ndugu zao ambao walikuwa katika ndege hiyo ya Ethiopia Airlines 737 iliyokuwa katika safari zake za kawaida kuelekea Nairobi, Kenya Jumapili asubuhi.
Ujumbe wa Twitter
Office of the Prime Minister - Ethiopia ✔ @PMEthiopia
The Office of the PM, on behalf of the Government and people of Ethiopia, would like to express it’s deepest condolences to the families of those that have lost their loved ones on Ethiopian Airlines Boeing 737 on regular scheduled flight to Nairobi, Kenya this morning.
4,933 people are talking about this
Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Washington, DC.