Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:10

Somalia, Ethiopia za ahidi kushirikiana kiuchumi, kupambana na ugaidi


Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed, kushoto akimtambulisha Waziri Mkuu mpya wa Ethiopia Abiy Ahmed, katikati, kwa mawaziri wake huko Mogadishu, Somalia, Juni 16, 2018.
Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed, kushoto akimtambulisha Waziri Mkuu mpya wa Ethiopia Abiy Ahmed, katikati, kwa mawaziri wake huko Mogadishu, Somalia, Juni 16, 2018.

Ushirikiano wa kiuchumi, uwekezaji wa pamoja na kushirikiana katika kupambana na ugaidi vilikuwa ni vitu muhimu katika mkataba ambao ulifikiwa katika mkutano kati ya viongozi wa Somalia na Ethiopia huko Mogadishu.

Hatua 16 zilizoafikiwa ziliweza kufikiwa baada ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed wa Ethiopia kufanya ziara ya kushitukiza Mogadishu mapema Jumamosi.

Wakati usalama ukiwa umeimarishwa kwa kuwekwa majeshi maalum ya Somalia, Rais Mohamed Abdullahi Farmajo alikuwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Aden Adde, Mogadishu kumpokea Ahmed.

Farmajo alisema kuwa alikuwa amemwalika Waziri Mkuu wa Ethiopia kuja Mogadishu.

Mambo muhimu ambayo nchi hizo mbili zimeweza kukubaliana, viongozi hao wamesema wamefikia makubaliano kuondoa vizuizi vyote vya kibiashara na kiuchumi. Pia wataongeza na kuzidisha mafungamano ya kiuchumi kwa kutengeneza miundombinu kama vile bandari na barabara.

XS
SM
MD
LG