Ahmed alipokelewa uwanja wa ndege na Rais Mohamed Abdullahi Farmajo.
Katika ujumbe wa Twitter, Rais Farmajo amemwambia Waziri Mkuu wa Ethiopia
“Karibu Mogadishu mheshimiwa ni heshima kwetu kukupokea wewe na wajumbe waliofuatana na wewe. Na ninaamini kuwa utafurahia kuwepo nchini.”
Msimamizi wa wafanyakazi katika ofisi ya Waziri Mkuu ameandika katika ujumbe wa Tweet: “Waziri Mkuu Abiy ameleta ujumbe wa mshikamano na urafiki kati ya Ethiopia na wananchi wa Somalia wasio kata tamaa.”
Baada ya kupokelewa kwa gwaride la heshima uwanjani hapo, Ahmed alipelekwa ikulu mjini Mogadishu takriban kilomita 5 upande wa kaskazini wa uwanja wa ndege ambako viongozi hao wanafanya mazungumzo.
Ulinzi umeimarishwa kwa kuwekwa wanajeshi wa Somalia katika barabara kuu zote mjini Mogadishu. Barabara zote zinazoelekea Uwanja wa Ndege na Ikulu zimefungwa.