Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 12:25

Watu 24 wamefariki kwa kimbunga Idai huko Zimbabwe


Kimbunga Idai kilichopiga Zimbabwe
Kimbunga Idai kilichopiga Zimbabwe

Idadi ya watu waliopotea hadi sasa ni 40 na vifo vinajumuisha wanafunzi wawili ilieleza wizara ya habari ya Zimbabwe kupitia Twitter. Kimbunga Idai pia kimeleta madhara nchini Msumbiji na Malawi

Wizara ya habari nchini Zimbabwe ilisema Jumamosi watu takribani 24 wamekufa huko kusini-mashariki mwa Zimbabwe ambapo nyumba na madaraja yamesombwa na dhoruba la msimu.

Kimbunga Idai ambacho kilisababisha mafuriko na uharibifu kwenye maeneo kadhaa nchini Msumbiji na Malawi kilipiga huko Zimbabwe siku ya Ijumaa na kusababisha umeme kukatika na mawasiliano mengine. Idadi ya vifo inathibitishwa kuwa ni 24 na vifo vingi ni kutoka eneo la Chimanimani mashariki. Idadi ya watu waliopotea hadi sasa ni 40 na vifo vinajumuisha wanafunzi wawili wizara hiyo ilieleza kupitia Twitter.

Madhara ya kimbunga Idai huko Zimbabwe na nchi za jirani
Madhara ya kimbunga Idai huko Zimbabwe na nchi za jirani

Wakati huo huo mbunge wa mashariki mwa wilaya ya Chimanimani, Joshua Sacco aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba kimbunga kimesababisha mifululizo ya uharibifu inayokumbusha kimbunga Eline kilichotokea Februari mwaka 2000 ambacho kiliharibu maeneo ya kusini mwa Zimbabwe. Sacco alisema idadi ya vifo ilitarajiwa kuongezeka wakati maafisa wakiendelea kutathmini hali ya tukio.

Eneo la Chimanimani linalopakana na Msumbiji limekuwa likiathiriwa vibaya na dhoruba linalosababisha mafuriko pamoja na kuharibu mazao, wizara ya habari nchini Zimbabwe ilieleza.

XS
SM
MD
LG