Wachunguzi kutoka shirika la Boeing na Mamlaka ya uchunguzi wa safari Marekani NTSA wamekwenda nchini Addis Ababa, Ethiopia kushiriki katika uchunguzi wa ajali hiyo.
Ndege hiyo mpya aina ya 737 Max 8 ilianguka dakika sita tu baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Bole kuelekea Nairobi, karibu na mji wa Bishoftu.
UNEP
Mkutano wa kimataifa wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Matiafa, UNEP, umefunguliwa mjini Nairobi kwa kukaa kimya kwa dakika moja ukitoa heshima kwa abiria 157 waliouawa katika ajali ya ndege ya shirika la Ethopian airlines.
Joyce Msuya Kaimu mkurugenzi mtendaji wa UNEP. ameeleza masikitiko yake na kutoa rambi rambi kwa familia za waliopoteza maisha na wale wote waliyohusika na msiba huo.
Kulikuwepo na watumishi 19 wa Umoja wa Mataifa waliokuwa wanaelekea Nairobi kuhudhuria mkutano huo wa baraza kuu la UNEP.
Ajali Indonesia
Ndege kama hiyo ya shirika la ndege la Lion ya Indonesia ilianguka mwezi Oktoba, 2018, muda mfupi baada ya kuruka.
Kazi za kutafuta miili ya abiria zinaendelea. Vyanzo vya habari vinasema kuwa wachunguzi wameanza kazi yao.
Kenya ilivyoathirika
Taarifa kutoka Kenya zinasema kuwa nchi hiyo imepoteza raia wake 32.
Kutokana na ajali hiyo, kumefunguliwa kituo cha kuwafariji wafiwa na kuwapa ushauri nasaha familia za watu waliopoteza ndugu zao.
Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Washington, DC.