Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 10:01

Antonio Guterres amesifia uchaguzi na juhudi za amani Afrika


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres

Guterres akiwa nchini Ethiopia alisema Afrika inakuwa mfano kwamba inawezekana kutatua na kuzuia mizozo na ninamatumaini upepo huu unaweza kuendelezwa kwenye maeneo mengine ya dunia.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres alisema Jumamosi kwamba chaguzi zilizofanyika kwa amani na maridhiano huko Afrika zilikuwa ishara za upepo wa matumaini kwenye bara hilo.

Guterres alikuwa anazungumza pembeni ya mkutano wa Umoja wa Afrika katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, mahala ambako wakuu wa nchi kutoka mataifa wanachama 55 watakutana kuanzia Jumapili. “Huu ni wakati ambapo upepo wa matumaini unavuma kote Afrika. Tumeshuhudia maridhiano kati ya Ethiopia na Eritrea, tumeshuhudia mikataba ya amani huko Sudan Kusini na Jamhuri ya Afrika ya kati-CAR, alisema Guterres.

Mwaka jana Ethiopia na Eritrea walimaliza vita baridi vilivyodumu miongo miwili wakati Sudan Kusini inajaribu kutekeleza makubaliano ya karibuni ya amani yaliyosubiriwa kwa muda mrefu ili kumaliza mgogoro wa miaka mitano ya umwagaji damu. Jamhuri ya Afrika ya kati-CAR wiki hii ilifikia makubaliano ya amani kati ya serikali na makundi 14 ya wanamgambo ikiongeza matumaini ya kumaliza matatizo ambayo yameikabili nchi hiyo tangu mwaka 2012 na kuzusha mzozo ambao umesababisha vifo vya maelfu ya watu na zaidi ya watu milioni moja kukoseshwa makazi.

Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa
Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa

“Matukio haya yote yamefanikiwa kupitia juhudi za pamoja za Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kuhakikisha mizozo ya bunduki itasitishwa kutoka mwaka 2020 na kuendelea kwenye bara la Afrika, alisema Guterres. Aliendelea kusema “ninaamini Afrika inakuwa mfano kwamba inawezekana kutatua mizozo na kuzuia mizozo na ninamatumaini upepo huu unaweza kuendelezwa kwenye maeneo mengine ya dunia”.

XS
SM
MD
LG