Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:10

Je, el-Sissi atakandamiza mifumo ya haki za binadamu iliyoko AU?


Rais Paul Kagame wa Rwanda aliyemaliza muda wake wa uwenyekiti katika Umoja wa Afrika.
Rais Paul Kagame wa Rwanda aliyemaliza muda wake wa uwenyekiti katika Umoja wa Afrika.

Wakati Rais wa Misri Abdel-Fattah el-Sissi akiwa amechaguliwa mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) katika kilele cha mkutano wa umoja huo nchini Ethiopia, Amnesty International inafikiri mifumo ya haki za binadamu iko mashakani katika umoja huo.

Kikundi hicho cha kutetea haki za binadamu kimeonya kuwa uwenyekiti wa el-Sissi unaweza kukandamiza mifumo iliyokuwa tayari imetengenezwa ya utetezi wa haki za binadamu ya Umoja wa Afrika.

Kikundi hicho cha haki za binadamu kimesema Misri tangu mwaka 2015 imeendeleza mipango ya mashambulizi ya kisiasa dhidi ya Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Umma, ACHPR, chombo ambacho kinalenga kufanya uangalizi juu ya rikodi za haki za bindamu katika nchi za Kiafrika.

“Dazeni za kesi zenye madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu uliopita kiwango zimefunguliwa dhidi ya Misri katika Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Umma” imesema Amnesty International.

Kuchaguliwa kwa El-Sisi kumehitimisha uwenyekiti wa mwaka moja wa Rais wa Rwanda Paul Kagame.

Wachambuzi wa kisiasa wanasema kuwa takriban imepita miaka sita tangu AU kuiweka kando, Misri mwaka 2013. Kurudi kwa Misri kunatabiriwa kuwa itachukua fursa hiyo kuimarisha madaraka yake.

Kuwekwa kando kulikuja baada ya jeshi la Misri kumuondoa madarakani rais Mohamed Mursi, ambaye mwaka 2012 alikuwa rais wa kwanza nchini humo aliyechaguliwa kidemokrasia.

Katika yale yaliyotajwa kuwa katika ajenda ya mkutano huo ni mizozo kadhaa ya bara hiyo ya kiusalama, pendekezo la Rwanda la kupata mfuko wa kugharamia bajeti ya bara hilo.

XS
SM
MD
LG