Mkutano huo maalum utafanyika katika makao makuu wa Umoja huo mjini Addis Ababa Jumamosi na Jumapili kwa msisitizo wa rais wa Rwanda Paul Kagame, ambaye amekuwa akiongoza shinikizo kuhusu mageuzi hayo.
Mabadiliko yanalenga kuuboresha na kuuwezesha Umoja wa Afrika - ambao ni wito wenye nguvu kwa muungano huo, ambao mara nyingi unaonekana kuwa usiyo na uwezo na unaotegemea zaidi wafadhili, na wadadisi wanasema muda wa kupatikana makubaliano ni mfupi.
Misri inatarajiwa kuchukua usukani mapema mwaka ujao, na wachambuzi wansema haionekani ikiwa na nia ya kuunga mkono mageuzi kwenye umoja huo.
Afrika Kusini, Zimbabwe, Botwana, Comoro, Togo na Ghana zimethibitisha kwamba zitawakilishwa na marais wao.