Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 17:03

Rais Kagame achukuwa uwenyekiti EAC


Rais wa Rwanda Paul Kagame amekubali kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na amewashukuru marais wenzake kwa kumpa dhamana hiyo na kuahidi kutumikia nafasi hiyo ipasavyo.

Amesema; “ninayo heshima kutumikia nafasi hii kwa kipindi cha mwaka mmoja. Natarajia kufanya kazi kwa ushirikiano wa pamoja na viongozi wenzangu kuwatumikia watu wa Afrika Mashariki.

Katika hotuba yake ya kupokea uongozi huo, Mwenyekiti mpya amemshukuru Rais Yoweri Museveni wa Uganda, ambaye amemaliza muda wake baada ya kuwa mwenyekiti wa marais wa nchi za Afrika Mashariki kwa kipindi cha miaka miwili.

“Napenda kuwaaeleza kuwa tuko pamoja na Rais Kenyatta na watu wa Kenya katika kupambana na ugaidi Afrika Mashariki,” ameeleza Kagame

“Hii ni fursa ya kuweza kukabiliana na changamoto zilizo kuwepo moja kwa moja ambazo zinaikabili jumuiya na kwa ukweli, ili sote kwa pamoja tuweze kusonga mbele.”

Mwenyekiti amesema kuwa jumuiya itaweza kupima mafanikio yake kwa namna ambayo watu, bidhaa na mitaji yao itakavyoweza kuingia katika nchi hizi na jinsi watakavyo weza kupata mafanikio kutokana na ushirikiano huo.

“Hili ni jukumu letu. Najua sote tuko sawa katika hili, iwapo tutaelekeza nguvu zetu zote ili kulifanisha hili.”

Kagame amesisitiza kwamba jumuiya isikubali kurudishwa nyuma katika hatua ya ushirikiano ambayo nchi zimekubaliana kwa maslahi ya pamoja, ikiwemo biashara, miundombinu, viwanda na usalama.

“Hatuwezi kuruhusu kurudi nyuma hasa wakati EAC imeanza kupiga hatua nzuri, ni juu yetu kuhakikisha Jumuiya inafanya kazi ipasavyo.

Ameongeza kuwa Afrika inapiga hatua kwa kuungana zaidi, kama ilivyo kwa Jumuiya za Kiuchumi za maeneo mengine, ambayo ni muhimu kwa kujenga umoja unaounganisha bara la Afrika.

“Mkutano huu wa marais umekuja wakati muhimu sana ambapo tunatarajia kuadhimisha miaka 20 tangu kufufuliwa upya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kuna mengi ya kusheherekea. Lakini pia ni wakati wa kutafakari juu ya thamani na umuhimu wa Jumuiya hii ambayo ni muhimu kwetu sote,” ameeleza Kagame

XS
SM
MD
LG