Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 14:49

Kenyatta : 'Hakuna anayeiba mali ya umma atakaye nusurika '


Rais Uhuru Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kwamba vita dhidi ya ufisadi nchini Kenya vitafaulu kupitia juhudi zote na kwamba havina msukumo wowote wa kisiasa.

Katika mahojiano ya kipekee na Sauti ya Amerika, Kenyatta amewataka wakenya wote kutoingiza siasa katika juhudi zilizopo za kukabiliana na ufisadi, akisisitiza kwamba hakuna mtu yeyote anayeiba mali ya umma atakaye nusurika katika vita hivyo.

Rais Kenyatta vile vile amekiri kwamba nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zinakabiliwa na mzozo wa kibiashara lakini akaeleza kwamba mizozo ni sehemu ya ustawi na kwamba jumuiya hiyo itafaulu katika malengo yake ya umoja na maendeleo.

Ametaja mzozo wa kibiashara kati ya mataifa ya EAC hasa baina ya Kenya na Tanzania, kuwa wa kawaida, unaotatulika kupitia mazungumzo.

Wakati huo huo Rais Uhuru Kenyatta amefanya mazungumzo na mwenzake wa Marekani Donald Trump, kuhusu masuala ya usalama, uekezaji na uongozi bora.

Nchi ya Kenya inalenga kuimarisha biashara kati yake na Marekani, chini ya mpango wa biasahara bila ushuru wa AGOA.

Marekani inaorodheshwa katika nafasi ya tano kwenye orodha ya washirika wa kibiashara wa Kenya, na katika nafasi ya tatu kwa kununua bidhaa kutoka Kenya.

XS
SM
MD
LG