Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:20

Wanajeshi madaktari wa EAC wanajadili changamoto za afya zilizopo


Viungo bandia ni mojawapo ya changamoto za afya
Viungo bandia ni mojawapo ya changamoto za afya

Wanajeshi madaktari kutoka wizara za ulinzi kwenye mataifa ya jumuiya ya Afrika mashariki wamekutana mjini Kigali nchini Rwanda kujadili changamoto za afya na huduma ya matibabu kwenye majeshi ya nchi zote sita za jumuiya ya Afrika mashariki

Wengi wa wajumbe hao ni maafisa wa jeshi wenye taaluma ya udaktari wanaohudumu kwenye majeshi ya nchi wanazotoka.

Brigedia Generali Katsigazi Tumusiime mwakilishi mwandamizi wa kijeshi kwenye makao makuu ya jumuiya Afrika mashariki akiiwakilisha Uganda. “Inawezekana kwamba endapo tutaungana chini ya mtazamo mmoja kama jumuiya ya Afrika mashariki tunaweza kuzitatua changamoto hizi za afya kwenye majeshi yetu. Hapa Rwanda tumeshuhudia mambo mengi yanayofanywa lakini pia nchi nyingine zimefanya kazi kubwa lakini mambo yanaweza kuwa mazuri zaidi tukiungana na kufanya kazi pamoja”.

Wanajeshi hawa wanakutana huku kukiwepo na kupungua kwa kasi ya utekelezaji wa mikataba kwenye itifaki mbalimbali ambazo kimsingi nchi zote ziliweka saini miaka iliyopita. Wengi wanakiri kwamba kwa upande wa wanasiasa kumekuwepo na hali ya kusuasua katika utekelezaji mikataba lakini kwa upande wa jeshi mambo ni tofauti kabisa. Aliendelea kusema Brigedia Generali Katsigazi Tumusiime. Kihistoria kumekuwepo na hali hii kwamba wanasiasa wamekuwa wakisuasua katika kutekeleza mikataba mbalimbali lakini kwa wanajeshi hii ni habari nyingine wanajeshi ni watu wanaozingatia nidhamu na muda wa kuweka mambo sawa, na chini ya mikataba ya ulinzi na usalama iliyopo baina yetu ni dhahiri kwamba haya tunayofanya hapa yatatekelezwa haraka iwezekanavyo”.

Mojawapo ya mashine za utabibu CT Scan
Mojawapo ya mashine za utabibu CT Scan

Kile kilichobainika ni kwamba kila nchi ina changamoto zake kwenye sekta ya afya na tiba kwa ujumla kwenye jeshi lake ikiwa ni pamoja na ukosefu wa watalaam wa kutosha, vitendea kazi na hata teknolojia ya kisasa. Haya yote wanajeshi hawa madaktari wanasema yatapatiwa jawabu kupitia ushirikiano wao.

Maafisa hawa wa kijeshi wanasema kuungana kwao kutakuwa na manufaa makubwa kwenye majeshi ya nchi zao kwa sasa watakuwa wameunganisha nguvu pamoja na utalaam wao.

Wakati huo huo Kanali Paul Bitega mkuu wa hospitali ya kijeshi nchini Rwanda. Alielezea zaidi lengo la wataalamu hao kukutana pamoja. “Lengo hasa ni kuainisha mambo na unapoainisha maana yake unafanya kazi pamoja na wengine. Hii ina maana kwamba mwanajeshi wetu kwa mfano akipata tatizo anaweza kupata matibabu kule Tanzania au Kenya au hata wao wakiwa na shida wanaweza kuja hapa maana yake tunakata kufanya mambo katika viwango sawa kwenye majeshi yetu yote”.

Wanajeshi wanatazamiwa kuandika ripoti ya pamoja baada ya mkutano wao wa faragha kisha kuifikisha ripoti hiyo kwenye kikao cha mawaziri wa ulinzi wa nchi hizo kitakachofanyika siku za hivi karibuni.

XS
SM
MD
LG