Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:10

Mgogoro wazuka kwenye uchaguzi wa spika wa jumuiya ya EAC


Makao makuu ya jumuiya ya Afrika Mashariki mjini Arusha, Tanzania.
Makao makuu ya jumuiya ya Afrika Mashariki mjini Arusha, Tanzania.

Mvutano mkubwa uliibuka Jumatatu mjini Arusha, Tanzania, kuhusu ni wajumbe wa nchi zipi waliofaa kusimama ili kuchaguliwa kama spika wa bunge la jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mgogoro huo ulizuka pale Tanzania, Burundi na Rwanda ziliposimamisha wajumbe wao huku nchi zingine wanachama wa jumuiya hiyo zikipinga hatua hiyo.

Baadhi ya wajumbe walisema kwamba baadhi ya nchi zilizotaka kusimamisha spika hazikuwa na nia njema kwa sababu wajumbe wao walikuwa wamehudumu kama spika katika mabunge ya zamani na hivyo basi ilikuwa ni zamu ya nchi zingine kuwasimamisha wajumbe wao.

Mwanahabari wa idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika, Sunday Shomari, alizungungumza kwa njia ya simu na aliyekuwa waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Tanzania, Dkt Diodorus Kamala, na kwanza akamuuliza sheria za jumuiya hiyo zinaelezaje kuhusu uchaguzi wa spika:

XS
SM
MD
LG