Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 15:13

Kimbunga Idai : Waliopoteza maisha Zimbabwe, Msumbiji wafikia 300


Idadi ya waliofariki kutokana na mafuriko yaliyo sababishwa na kimbunga kikali cha Idai huko Msumbiji na Zimbabwe imefikia 300, huku waokozi wakifanya kila wanaloweza kuwaokoa walionusurika kutokana na mafuriko yaliyotokea katika nchi hizo.

Zaidi ya watu 150 wamethibitihswa kufa na mamia hawajulikani walipo kufuatia kimbunga Idai, kilichopiga kusini mashariki mwa Afrika, mji wa Beira, nchini Msumbiji ambapo miundombinu yake yote imeharibika kabisa.

Umoja wa Mataifa unaeleza kwamba mamilioni ya watu wameathirika katika nchi tatu za kusini mwa Afrika na kwamba timu za uokozi na msaada wa dharura zinapelekwa huko kwa haraka. Umoja wa ulaya umetangaza msaada wa karibu dola milioni 4 kwa Msumbiji Malawi na Zimabwe . Uingereza nayo ikiahidi dola milioni 8.

Rais Emmerson Mnangagwewa Zimbabwe alitembelea jana wilaya ya Chimanimani na kusema kwamba mataifa ya kusini mwa afrika yameahidi kupeleka msaadawa dharura kwa haraka iwezekanavyo.

Waokozi katika maeneo ya mafuriko kati kati ya Msumbiji wanatumia boti kujaribu kuwaokowa watu walokwama juu ya miti na paa za nyumba.

Na wanajeshi wa majeshi ya anga ya Afrika Kusini na Msumbiji wamepewa jukumu la kutumia helikopta kuwaokowa watu.

Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi alisema Jumatatu kwamba kuna zaidi ya watu 200 waliofariki na laki tatu na nusu wako bado hatarini. Na kuongeza kusema huenda idadi ya waliopoteza maisha kutokana na janga hilo ikafikia elfu moja.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Abdushakur Aboud, Washington, DC

XS
SM
MD
LG