Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 15:18

Trump kuitoa Marekani nje ya Mkataba wa Paris


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Serikali ya Marekani itajiondoa kutoka kwenye mkataba wa hali ya hewa wa Paris, Rais Donald Trump ametangaza Alhamisi.

Hiyo ni moja ya ahadi yake kubwa aliyokuwa akiinadi wakati wa kampeni za urais lakini inahatarisha juhudi za ulimwengu katika kupambana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

Katika sherehe iliofanyika kwenye bustani ya Rose Garden ya ikulu ya White House katika siku yenye joto kali Alhamisi, Trump amesema mkataba umesaidia kidogo sana mazingira na kuiadhibu bila ya haki yoyote Marekani kwa kuilazimisha ikubaliane na masharti magumu sana kuliko nchi nyingine zinazoharibu mazingira.

“Mkataba wa Paris ni mfano mdogo tu wa hivi karibuni wa Washington kuingia katika mkataba ambao unaikandamiza Marekani kwa maslahi yanayo wanufaisha tu nchi nyingine,” amesema Trump.

Hatua hiyo inakuja pamoja na kuwepo juhudi za wale wenye kupinga kwa dhati maamuzi ya Trump, kutoka katika makundi ya viongozi wa ulimwengu na wafanyabiashara, wengi ambao walikuwa wamemuomba rais wao katika siku za hivi karibuni kuendeleza mkataba wa hali ya hewa.

Mwisho wa yote, Trump ametupilia mbali mkataba huo akikinzana na jaribio la “washawishi wa kigeni” ambao wanataka Marekani “kulazimika na kujizuia” ili kwamba nchi zao ziwe na maslahi zaidi ya kiuchumi.”

“Nilichaguliwa ili kuwawakilisha wananchi wa Pittsburgh na siyo Paris,” amesema Trump

Makubaliano yaliofikiwa 2015, yameweka malengo ya kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa unatokana na viwanda na kudhibiti kuongezeka kwa joto duniani, ambayo ilisianiwa na nchi 195.

XS
SM
MD
LG