Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 02:28

EU, China zaahidi upya kuulinda mkataba wa Paris


Rais wa Baraza la Ulaya Donald Tusk, Waziri Mkuu wa China Li Keqiang na Rais wa Tume ya EU Jean-Claude katika mkutano Brussels
Rais wa Baraza la Ulaya Donald Tusk, Waziri Mkuu wa China Li Keqiang na Rais wa Tume ya EU Jean-Claude katika mkutano Brussels

Umoja wa Ulaya (EU) na China umeahidi tena Ijumaa kuendeleza mkataba wa hali ya hewa wa Paris 2015, siku moja baada ya Marekani kutangaza kujitoa katika makubaliano hayo.

Katika mkutano wa pamoja, EU na China zimesema mabadiliko ya hali ya hewa na nishati safi “itakuwa ni nguzo yao muhimu” katika ushirikiano wao.

Rais wa Baraza la Ulaya Donald Tusk amesema juhudi za kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa zitaendelea, bila ya kujali kuwepo au kutokuwepo kwa Marekani:

“Leo, China na EU umeonyesha mshikamano wao kwa kushirikiana na kizazi kijacho na majukumu ya kusimamia dunia yote,” amesema. “Tunaamini kuwa uamuzi uliofanywa jana ni kosa kubwa.”

Waziri mkuu wa China Li Keqiang, akiwa Brussels kwa ajili ya mkutano wa kibiashara kati ya Umoja wa Ulaya na China, amesema ni jambo la muhimu kwa mahusiano ya China na EU kuimarishwa zaidi.

“Tunaamini kuwa kumekuwa na mabadiliko katika medani za kimataifa, na kutaendelea kuwepo mashaka na sababu zakutuyumbisha,” amesema. “Hili linatutaka tuongeze juhudi zetu ilikutatua mambo haya yanayotukabili.”

XS
SM
MD
LG