Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 02:55

Baghdad : Maelfu wahudhuria mazishi ya Jenerali aliyeuawa na Marekani


Waombolezaji wahudhuria maziko ya Meja Jenerali wa Iran Qassem Soleimani, na kamanda wa wanamgambo wa Iraq Abu Mahdi al-Muhandis Iraq, REUTERS/Khalid al-Mousily
Waombolezaji wahudhuria maziko ya Meja Jenerali wa Iran Qassem Soleimani, na kamanda wa wanamgambo wa Iraq Abu Mahdi al-Muhandis Iraq, REUTERS/Khalid al-Mousily

Maelfu ya waombolezaji walikusanyika Jumamosi katika maandamano ya maziko yaliokatiza mjini Baghdad ya jenerali wa ngazi ya juu wa Iran na kiongozi wa wanamgambo wa Iraqi waliouawa katika shambulizi la anga ambalo limepelekea mgogoro wa eneo hilo kuongezeka.

Jenerali Qassem Soleimani, mkuu wa kikosi maalum cha Quds na mtayarishaji wa mkakati wa usalama wa eneo hilo, aliuawa katika shambulizi la anga mapema Ijumaa karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa uliopo makao makuu ya Iraq.

Soleimani ndiye aliyekuwa mpangaji wa sera ya Iran katika eneo hilo akiwakusanya wanamgambo kote nchini Iraq , Syria na Lebanon, ikiwemo vita dhidi ya kikundi cha Islamic State.

Pia analaumiwa kufanya mashambulizi dhidi ya majeshi ya Marekani na washirika wake tangu wakati Marekani ilipoivamia Iraq mwaka 2003.

Waombolezaji wengi waliokuwa wamevalia vazi jeusi, na kubeba bendera ya Iraqi na bendera ya wanamgambo wanaosaidiwa na Iran ambao ni waaminifu kwa Soleimani.

Pia walikuwa wanaomboleza kifo cha Abu Mahdi al-Muhandis, kamanda wa ngazi ya juu wa wanamgambo wa Iraqi ambaye aliuawa katika shambulizi hilo pia.

XS
SM
MD
LG