Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:04

Wachambuzi wasema mdahalo kati ya Harris na Pence una mvuto mkubwa


Seneta Kamala Harris (kulia) na Makamu wa Rais Mike Pence.
Seneta Kamala Harris (kulia) na Makamu wa Rais Mike Pence.

Macho ya Wamarekani wengi hii leo yanaelekea mjini Salt Lake ambako Makamu wa Rais Mike Pence na mgombea mwenza wa chama cha Demokratik Seneta Kamala Harris wanakutana katika mdahalo muhimu wa kampeni za uchaguzi wa Novemba 3.

Mdahalo umekuwa muhimu kutokana na jinsi mdahalo kati ya wagombea urais ulivyoendelea wiki iliyopita pamoja na hali ya afya ya Rais Donald Trump.

Rais Donald Trump na Makamu wa Rais wa zamani Joe Biden
Rais Donald Trump na Makamu wa Rais wa zamani Joe Biden

Wachambuzi wa mambo wanasema mdahalo huu unaofanyika Salt Lake City ni muhimu kabisa kutokana na taifa la Marekani kuwa limegawika kuhusiana na masuala ya kiuchumi, janga la corona na suala la ubaguzi wa rangi.

Raphael Sonenshein wa Chuo Kikuu cha California State anasema watu wengi watataka kutizama mdahalo kwa vile wagombea kiti cha rais ni wazee wawili.

Sonenshein katika mahojiano kwa njia ya Skype anasema : Inamkumbusha kila mtu kwamba kuna mgombea mwenye umri wa miaka 74 anaeshindania kiti cha rais dhidi ya mwengine mwenye umri wa miaka 77, na kuna vijana wawili mmoja ni makamu rais na mwengine ni mgombea mwenza ambao wanaweza kwa urahisi kuwa wagombea urais uchaguzi ujao.

Mitchell McKinney mkurugenzi wa taasisi ya mawasiliano ya kisiasa katika Chuo Kikuu cha Missouri anasema mdahalo wa Jumatano kati ya Makamu wa Rais Mike Pence Mrepublikan na Mdemokrat Seneta Kamala Harris unamambo mengi ya kuvutia kuwafanya watu kutaka kuutizama.

McKinney anafafanua kwa kusema : Kutokana na tukio la kihistoria la kuteuliwa kwa Kamala Harris kuwa ni mwanamke mweusi wa kwanza katika kinyang'anyiro hichi na kushiriki kwenye mdahalo.

Kwani mwanamke wa kwanza kushiriki kwenye mdahalo wa wagombea wenza alikuwa ni Geraldine Ferraro alipokabiliana na George Herbert Bush mgombea mwenza wa Ronald reagan mwaka 1984.

Halafu mara ya pili wapiga kura wakawa na hamu kweli ya kuona jinsi Sarah Palin anavyopambana na Joe Biden.

McKinney pia anaeleza kuwa matarajio ya mdahalo wa makamu rais kati ya Biden na Palin yalikuwa makubwa, ilikuwa wakati pekee katika historia ya midahalo ya rais ambapo mdahalo wa nafasi ya makamu rais kutizamwa na watu wengi kuliko hata mdahalo wa wagombea urais wenyewe.

Na hivyo hii leo kutokana na Rais Trump kuugua Covid -19 matarajio yamekua juu zaidi kwa ajili ya mdahalo kati ya Pence na Harris.

Hivyo Alan Schroeder wa Chuo Kikuu cha Northeastern anasema huenda wote watakuwa wakilenga kugombania uchaguzi ujao.

Schroeder anafafanua :" Ikiwa Pence atafanya tena vizuri katika mdahalo wa 2020, kama alivyofanya miaka minne iliyopita basi hiyo itamsaidia sana kupata nguvu kama mgombea wa chama cha Republikan kwa ajili ya mwaka 2024 na ni sawa pia kwa kamala Harris ambaye bila shaka ni kijana na ana ari ya muda mrefu.

Mbali na hayo Mary Kate Cary wa Chuo Kikuu cha Virginia anasema ni namna wanasiasa hao wawili wanavyofahamika katika kutoa hoja kwenye majadiliano ndio wanavutia zaidi. Harris aliyewahi kuwa mwendesha mashtaka ni hodari kupanga hoja na Pence aliyewahi kuwa Gavana na Mtangazaji wa redio ni mtulivu.

Cary anaeleza kuwa : Harris alipata umashuhuri kutokana na namna alivyokuwa akihoji watu kwa ustadi na nguvu. Anafahamu namna ya kuweka masuala ya mitego na kujaribu kumwekea mtu chambo kujibu. Hivyo atakuwa mbishani hodari. Na ninadhani Pence kwa upande mwengine si mtu rahisi kutambua hisia zake kwa namna alivyo mtulivu, hivyo haitakuwa rahisi kuingia kwenye mtego,

Basi mdahalo huo utakaguliwa kwa kina na unafanyika chini ya masharti makali ya kupambana na janga la corona ambapo Pence na Harris watatengenishwa kwa umbali wa mita nne kukiwepo na vioo kati yao.

XS
SM
MD
LG