Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 02:25

Rais Trump, anayetibiwa COVID-19, kufanya kazi kutoka hospitali


Helikopta ikiondoka White House ikiwa imembeba Rais Donald Trump ikielekea Hospitali.
Helikopta ikiondoka White House ikiwa imembeba Rais Donald Trump ikielekea Hospitali.

Ijumaa usiku Rais wa Marekani Donald Trump, anayeuguwa COVID-19 alituma ujumbe wa Twitter kutoka hospitali, “Nafikiri, naendelea vizuri! Asanteni nyote. NAWAPENDA!”

Daktari wa Rais, Sean Conley, amesema katika waraka wake kwa msemaji wa White House Kayleigh McEnany Ijumaa. “Jioni hii ninafuraha kuripoti kuwa Rais anaendelea vizuri sana.Rais wa Marekani amelazwa kwa ajili ya matibabu ya COVID-19.

Hahitaji ziada yoyote ya hewa ya Oxygen, lakini kwa kushirikiana na madaktari bingwa tumeamua kuanzisha matibabu ya dawa ya Remdesivir. Tayari amemaliza dozi ya kwanza na anaendelea kupumzika vizuri.”

Trump alipelekwa kwa helicopter kutoka White House katika Hospitali ya Kijeshi ya Taifa ya Walter Reed iliyoko karibu na Washington. Alipokuwa akiondoka aliwapungia mkono waandishi na kuashirikia yuko vizuri. Hospitali alipo huko Bethesda Maryland inachumba kinacho wawezesha maraisi kufanya kazi kutoka hapo.

Yeye na mkewe, Melania Trump, wameambukizwa ugonjwa huo, lakini Melania anaendelea kupata nafuu akiwa White House.

Rais kutokana na jinsia yake, uzito wake na umri (74) imemuweka katika kundi la watu wenye kukabiliwa na hali hatarishi zaidi katika kutibu ugonjwa huu.

Trump hakuwa ni mwenye kuunga mkono uvaaji wa barakoa, ingawaje washauri wake wamesema kufanya hivyo ni njia ya kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo wa kuambukiza.

Watu kadhaa wanaomzunguka rais pia wamegundulika wana maambukizi ya COVID-19 baada ya kupimwa wiki iliyopita, akiwemo msaidizi wake wa ngazi ya juu Hope Hicks na msaidizi wake wa zamani Kellyanne Conway.

Kiongozi huyo wa Marekani amekuwa miongoni mwa viongozi wa dunia walioambukizwa ugonjwa huo, akiwemo Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, Rais wa Brazil Jair Bolsonaro, Rais wa Honduras Juan Orlando Hernandez, Rais wa Bolivia Jeanine Anez na kiongozi wa Armenia Nikol Pashinyan.

Gazeti la New York Times linaripoti kuwa kumekuwa na mlipuko wa virusi vya corona katika kituo cha mafunzo cha walinzi maalum (Secret Service) huko Maryland mwezi August.

Kituo hicho kilifungwa baada watu wasiopungua 11 waliokuwa wanafanya kazi hapo walipoambukizwa virusi hivyo.

Gazeti hilo limeripoti kuwa hakuna kiashiria chochote kuwa mlipuko huu ulipelekea maambukizi hayo kwa walinzi na maafisa ambao wanamlinda moja kwa moja rais.”

Secret Service ni walinzi maalum waliofunzwa kumlinda rais wa Marekani.

XS
SM
MD
LG