Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 02:21

COVID-19 : Viongozi wa dunia wamtakia Rais Trump na mkewe kupata nafuu haraka


Rais Donald Trump na mkewe Melania
Rais Donald Trump na mkewe Melania

Viongozi wa dunia wamekuwa wakituma ujumbe wa kuwaombea rais Donald Trump na mkewe Melania afya njema baada ya kutangazwa mapema Ijumaa kwamba wote wameambukizwa na virusi vya Corona.

Rais Trump aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba yeye na Melania wamepimwa na kupatikana na virusi vya Corona na watabaki katika hali ya karantina kwa muda wa wiki mbili.

Rais Trump alitoa habari hizo kwanza alipokuwa anahojiwa na kituo cha televisheni cha Fox na kusema walipimwa baada ya mshauri wake wa karibu Hope Hicks kuthibitishwa kwamba ameambukizwa na virusi hivyo.

Hope Hicks
Hope Hicks

Mara baada ya kutolewa ujumbe huo alfajiri ya siku ya Ijumaa viongozi kutoka pembe zote za dunia wamekuwa wakituma ujumbe wa kuwatakia heri na kupata afweni kwa haraka.

Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson ambaye ni moja kati ya viongozi wa dunia waliouguwa ugonjwa wa COVID-19 pamoja na rais wa Brazil Jair Bolsoaro walimuombea kupata afweni ya haraka.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson

Johnson alieleza : "Bila shaka ninadhani sote tunampelekea ujumbe wakumtakia kila la kheri rais na mke wake na tayari nimefanya hivyo leo asubuhi. Na nina hakika wote watapambana vyema na ugonjwa huo na kupata nafuu."

Mkurugenzi mkuu wa wa shirika la afya dunia Tedros Adhamon Ghebreyesus, kupitia ujumbe wa Twitter amewatakia Trump na Melania kupona haraka.

Habari hizi zimesababisha bei kushuka kwenye masoko ya hisa na kuzusha hofu juu ya hali itakavyo kuwa katika siku zijazo.

Bei katika masoko ya Ulaya na Asia zilishuka kwa wastani wa asilimia moja na soko la hisa la New York lilifunguliwa bei zikiwa chini ingawa wachambuzi wanasema bei zilikuwa chini tangu mwanzoni mwa wiki hii.

Na habari pia zimezusha wasiwasi juu ya kampeni za rais ikiwa imebaki mwezi mmoja kabla ya uchaguzi mkuu ambapo atapambana na Joe Biden aneongoza katika uchunguzi wa maoni.

Trump alikuwa amepanga kuwa na mikutano mikubwa ya hadhara Ijumaa hii hadi mwisho wa wiki lakini yote imeahirishwa kulingana na maafisa wa kampeni yake.

Biden amewatakia rais na mkewe wa[popne kwa haraka, mara baada ya kupata habari hizo.

Kabla ya kutangaza kwamba amepimwa na virusi vya corona Trump alitoa ujumbe wa matumaini hapo Alhamisi alipokuwa anahutubia kwa video tafrija ya kila mwaka ya 75 kuchangisha fedha kwa ajili ya watoto katika jiji la New York

Mike Pompeo
Mike Pompeo

Tunaomboleza vifo vya wale wote waliopoteza maisha yao. Na kwa ajili yao tutavishinda virusi hivi. Tuko katika njia nzuri ya kutengeneza na kusambaza chanjo kabla ya mwisho wa mwaka huu na pengine hata kabla ya mwisho wa mwaka.

White House imetoa taarifa Ijumaa ikieleza kwamba rais na mkewe wako katika hali nzuri na hakuna wasiwasi kwa wakati huu. Na kwamba makamu rais Mike Pence amearifiwa kuwa tayari kushika uongozi ikihitajika.

Kwa upande mwengine akiwa anarudi kutoka Rome Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani Mike Pompeo akiwatakia heri rais na mkewe aliwambia waandishi wa habari kwamba anatafakari hivi sasa juu ya kuahirisha ziara yake ya nchi za Asia hivi karibuni kutokana na habari hizo.

XS
SM
MD
LG