Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:53

Trump amteua Amy Coney Barrett kuwa jaji wa mahakama ya juu


Rais Donald Trump akitangaza uteuzi wa Jaji Amy Coney Barrett kwenye bustani ya Rose Garden ya Ikulu mjini Washington DC.
Rais Donald Trump akitangaza uteuzi wa Jaji Amy Coney Barrett kwenye bustani ya Rose Garden ya Ikulu mjini Washington DC.

Rais wa Marekani Donald Trump Jumamosi alimteua Amy Coney Barrett kuchukua nafasi ya jaji wa Mahakama ya Juu ilioachwa wazi kutokana na kifo cha Jaji mliberali Ruth Bader Ginsburg.

Trump alitangaza rasmi uteuzi huo katika hafla iliyofanyika kwenye bustani iitwayo Rose Garden, nje ya White House, ambayo ilihudhuriwa na darzeni kadhaa za watu.

Kifo cha Ginsburg kimempa fursa Trump kujaribu kuifanya mahakama iwe ya Waconservative zaidi chini ya wiki sita zijazo kabla ya uchaguzi wa rais kufanyika.

Iwapo ataidhinishwa, Jaji Barrett atakuwa mmoja wa majaji tisa kwenye mahakama hiyo ya juu kabisa.

"Jaji Emy Coney Barrett ni mmoja wa watu wenye vipaji vikubwa zaidi nchini. Nina imani mchakato wa kumuidhinisha utafanyika haraka," alisema Rais Trump.

"Ni fahari kubwa kwangu kuteuliwa na Rais Donald Trump kwa nafasi hii. Iwapo nitaidhinishwa, sitasahau yule aliyenitangulia...Jaji Ruth Bader Ginsburg kwa sababu alikuwa kielelezo cha kipekee," alisema Jaji Barrett.

Jaji Amy Coney Barrett
Jaji Amy Coney Barrett

Trump alikuwa ameahidi kumchagua mwanamke kumrithi Ginsburg, aliyefariki wiki iliopita akiwa na umri wa miaka 87.

Barrett, mwenye umri wa miaka 48, aliteuliwa katika mahakama ya rufaa ya serikali kuu kwa wilaya ya saba mwaka 2017 na kwa wakati mmoja, alihudumu kama mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Notre Dame.

Uamuzi wa rais Trump kufanya uteuzi kabla ya kinyang’anyiro cha urais chenye ushindani mkubwa kufanyika ili achaguliwe tena akishindana na Makamu wa Rais wa zamani Joe Biden kimesababisha mvutano wa kisiasa mkali mjini Washington.

Haya yanajiri wakati mvutano ukiendelea, viongozi Warepublikan katika
Baraza la Seneti wakidai mchakato wa kumthibitisha mteule huyo uendelee kwa haraka iwezekanavyo huku Wademokrat wakitaka uteuzi huo usubiri mpaka mshindi wa uchaguzi wa rais utakaofanyika Novemba atakapojulikana.

Shirika la habari la Fox, Jumamosi liliripoti kwamba maseneta 51 wamesema wataunga mkono uteuzi huo wa Jaji Barrett.

Amy Coney Barrett ni nani?

Alizaliwa Amy Vivian Coney tarehe 28 Januari mwaka wa 1972 katika mji wa New Orleans, Louisiana.

Alikuwa kati ya watoto saba kwenye familia yake, dada watano na kaka mmoja

Babake, Michael Coney alikuwa mwanasheria huku, mamake, Linda Coney akiwa mlezi wa watoto nyumbani.

Amy ameolewa na mwanasheria Jesse Barret na wana jumla ya watoto saba.

XS
SM
MD
LG