Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:08

WHO: Chanjo ya Covid-19 inaweza kupatikana mwishoni mwa mwaka huu


Mkurugenzi mkuu wa shirika la afya duniani WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus.
Mkurugenzi mkuu wa shirika la afya duniani WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus.

Chanjo ya virusi vya corona inaweza kupatikana mwishoni mwa mwaka huu, kwa mujibu wa mkuu wa shirika la afya duniani WHO.

Mkurungenzi wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, ametoa wito wa mshikamano na dhamira ya kisiasa kwa viongozi wote, ili kuhakikisha kwamba chanjo zitatolewa kwa usawa.

“Tunahitaji chanjo, na kuna matumaini kwamba mwishoni mwa mwaka tunaweza kupata chanjo. Hakika kuna matumaini," amesema Tedros, katika hotuba ya kufunga kikao cha bodi cha uongozi wa WHO.

Chanjo tisa za majiribio ziko kwenye ratiba ya kituo cha chanjo cha kimataifa cha WHO, COVAX, ambacho kinakusudia kusambaza dozi billioni 2 kufikia mwisho mwa 2021.

Mkutano huo wa siku mbili wa bodi ya uongozi wa WHO, ulichunguza namna ulimwengu unavyopambana, na janga la Covid-19, na ulisikia wito kutoka Ujerumani, Uingereza na Austria, kuhusu kuimarisha shirika hilo la umoja wa mataifa.

Utawala wa rais wa Marekani, Donald Trump, uliikosoa WHO namna inavyoshughulikia janga hili.

Pia umeshutumu WHO, kushirikiana na China, na haikutekeleza jukumu lake kwa kuiwajibisha juu ya vitendo vyake, wakati virusi vya corona vilipoanza kwa mara ya kwanza mwaka uliopita.

Lakini Tredros alitupilia mbali madai hayo ya Marekani, na kusema kwamba WHO, iliendelea kutoa taarifa kwa ulimwengu.

XS
SM
MD
LG