Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 27, 2024 Local time: 05:48

Wafuasi wa Trump na Biden hawatakubali matokeo ya uchaguzi- ukusanyaji maoni


Rais Donald Trump, kushoto, na aliyekuwa makam wa rais Joe Biden, Kulia.
Rais Donald Trump, kushoto, na aliyekuwa makam wa rais Joe Biden, Kulia.

Ukusanyaji wa maoni ulioendeshwa na shirika la habari la Reuters kwa ushirikiano na taasisi ya Ipsos umeonyesha kuwa zaidi ya wafuasi wanne kati ya kumi wa rais Donald Trump na mpinzani wake Joe Biden, wamesema hawatokubali matokeo ya uchaguzi wa Novemba iwapo mgombea wanayemuunga mkono atashindwa.

Utafiti huo ambao uliendeshwa kati ya tarehe 13 na tarehe 20 Oktoba unaonyesha asilimia 43 ya wafuasi wa Biden hawatokubali ushindi wa Trump, na asilimia 41 ya wale wanaotaka Trump achaguliwe kwa muhula wa pili hawatokubali ushindi wa Biden.

Asilimia 22 ya wafuasi wa Biden na asilimia 16 ya wafuasi wa Trump wamesema wako tayari kufanya maandamano hata kujihusisha na vitendo vya vurugu iwapo mgombea wanayemuunga mkono atashindwa.

Maafisa wanaosimamia uchaguzi wanakabiliwa na changamoto nyingi mwaka huu na walielezea wasiwasi wao kuhusu Imani ya umma juu ya matokeo ya uchaguzi.

Imetayarishwa na Patrick Nduwimana, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG