Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:59

Waafrika wafuatilia matokeo ya uchaguzi wa Marekani kwa kejeli


Wakaazi katika mataifa mbalimbali ya Afrika wanaendelea kufuatilia matokeo ya uchaguzi mkuu wa Marekani kwa hisia tofauti zilizojaa kejeli na hali ya kutoamini hasa baada ya rais Donald Trump kujaribu kujitangaza mshindi wa uchaguzi huo kabla ya hesabu ya kura kukamilika.

Katika baadhi ya nchi za Afrika ambazo uchaguzi umefanyika hivi karibuni na kukumbwa na utata wa matokeo kama Guinea, baadhi ya raia wameeleza kusikitishwa na rais Trump kudai ushindi wakati hata hesabu ya kura ilikuwa inaonyesha kwamba alikuwa nyuma ya Joe Biden.

Mory Keita, ambaye ni raia wa Guinea, amesema kwamba rais Trump anaonyesha mfano mbaya sana kwa nchi za Afrika ambazo bado ni changa kidemokrasia, huku Bachir Diallo akisema kuwa hatua ya Trump ni ya kuleta fedheha sana kwamba hayo ni mambo ambayo yanatarajiwa kutokea katika nchi yenye utawala mbovu sana na wala sio Marekani.

Kura zinaendelea kuhesabiwa katika uchaguzi wa Marekani, Joe Biden akiwa anaongoza kwa idadi ya kura, lakini hakuna mshindi amepatikana hadi sasa.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG