Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:21

Baraza la Wawakilishi latarajiwa kuwasilisha azimio la kumuondoa Rais Trump madarakani


Spika Nancy Pelosi
Spika Nancy Pelosi

Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani Nancy Pelosi amesema baraza hilo litawasilisha Jumatatu azimio la kutaka Baraza la Mawaziri la Rais Donald Trump kutumia kipengele cha 25 cha katiba ya Marekani, ambacho kinapendekeza rais aondolowe madarakani inapodhihirika kuwa hafai kuendelea kuliongoza taifa.

Katika barua aliotuma kwa wabunge wa chama cha wa Demokratik, Pelosi alisema iwapo Makamu Rais Mike Pence hatajibu ombi hilo katika muda wa saa 24, Baraza la Wawakilishi litaanzisha mchakato wa kumfungulia mashtaka ya kumuondoa madarakani Rais Trump.

Shinikizo la kutaka Rais Trump aondolewe madarakani linakuja wakati wito wa kutaka awajibishwe kwa kuhusika na uvamizi wa jengo la bunge la Marekani Jumatano wiki iliopita, unazidi kuongezeka. Watu watano wamepoteza maisha kufuatia uvamizi uliofanywa na wafuasi wa Trump katika jengo hilo.

Kufikia jana Jumapili, Trump wala White House walikuwa hawajajibu kuhusu ombi la Pelosi.

XS
SM
MD
LG